Yassir Simba, Michuzi Tv

Mchezo wa nne wa robo fainali wa kombe la Azam Sports Federation umepigwa leo katika dimba la Uwanja wa Taifa Maarufu kama kwa Mkapa ikiwakutanisha  mabingwa mara tatu mfululizo wa ligi kuu Tanzania bara Simba Sports Club dhidi ya Azam Fc.

Mchezo huo ulioamuriwa kwa mabao ya Papa John Rafael Bocco katika dakika ya 39 ya mchezo na bao la mwamba wa Lusaka Clatous Chota Chama katika dakika ya 56 ya mchezo ilitosha kuwaondoa waoka mikate wa Chamazi Azam Fc.

Mchezo huo uliotawaliwa na Simba Sports Club kwa asimilia kubwa ulitosha kuwafungasha virago Azam Fc katika hatua ya robo fainali ya ASFC.

Katika mchezo huo pia ilishuhudia Simba ikilazimika kumtoa beki wake aliyekuwa katika kiwango bora sana katika mchezo huo Kennedy Juma aliyeumia mwishoni mwa kipindi cha kwanza cha mchezo na nafasi yake kuchukuliwa na Erast Nyoni.

Mara baada ya matokeo hayo Simba anatinga nusu fainali ya ASFC  wakiungana na Sahare All Stars  ya mkoani Tanga mara baada ya kumtoa Ndanda Sports Club ya mkoani Mtwara katika mikwaju ya penalti kwa penalti 4 kwa 3.

Rasmi sasa Namungo FC,Yanga, Sahare All Stars  pamoja na Simba wanakwenda katika hatua ya nusu fainali ya kombe hilo la Shirikisho la Azam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...