Mkuu wa MKoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akifunga mafunzo maalum ya siku sita kwa wadau zaidi ya 300 kutoka katika mikoa mbalimbali nchini yaliyokuwa yameandaliwa na Baraza la Taifa la watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI (NACOPHA) kupitia “Mradi wa Hebu Tuyajenge” unaotekelezwa katika kipindi cha miaka mitano 2019-2024, unaofadhiliwa na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) katika mikoa 22 Tanzania Bara. kushoto Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Rahabu Mwagisa, Kulia Mkurugenzi wa Utatifi wa NACOPHA Pantaleo Shoki



Awataka wenye virusi kufanya kazi bila hofu

Awaonya wanaomchokoza,asisitiza hatatia nia


Na John Mapepele

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi amempongeza Rais Magufuli kwa kuvunja rekodi ya maendeleo kabla ya mwaka 2025 na kuifanya Tanzania kuingia kwenye nchi za uchumi wa kati duniani Julai Mosi mwaka huu.

Huku akiwahimiza watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI nchini kufanya kazi kwa bidii bila kuwa na hofu sambamba na kumtanguliza Mungu na kutumia fursa za mikopo inayotolewa na Serikali ya Awamu ya Tano ili ku kuinua hali za maisha na kuongeza pato la taifa kwa ujumla

Dkt. Nchimbi ameyasema hayo leo katika Mji Mdogo wa Manyoni mkoani Singida alipokuwa akifunga mafunzo maalum ya siku sita kwa wadau zaidi ya mia 3 kutoka katika mikoa mbalimbali nchini yaliyokuwa yameandaliwa na Baraza la Taifa la watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI (NACOPHA) kupitia “Mradi wa Hebu Tuyajenge”.

Mradi huo unaotekelezwa katika kipindi cha miaka mitano 2019-2024,unaofadhiliwa na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) katika mikoa 22 Tanzania Bara.

Amesema kwa sasa Serikali ya Awamu ya Tano imepiga hatua kubwa ya kupiga vita unyanyapaa dhidi ya watu wanaishi na virusi vya UKIMWI na kwamba watu wote wana haki na fursa sawa mbele ya Serikali yao hivyo hakuna sababu ya wao kuendelea kujinyanyapaa wenyewe na badala yake wawe walimu wa kuwaelimisha wengine kwenda kupima na kutambua hali zao na kuendelea kuchapa kazi ili kuinua uchumi wan chi yetu.

“Kubwa ndugu zangu hapa ni kumtanguliza Mungu mbele, kutoa hofu na kuachana na mambo yote ambayo yanapelekea kudhoofu kwa afya zetu kama vile unywaji wa pombe hata kama wake zetu wanapika kwa ajili ya biashara na badala yake tutumie juisi lishe za matunda ya asili kama vile Sasati, Ubuyu na Ukwaju” amesisitiza Dkt. Nchimbi

Umewaelekeza Wataalam wa Maendeleo ya Jamii wa Mkoa wa Singida kuangalia namna ya kuja na mikakati madhubuti ya kiuendelevu ya kuwakopesha wanaoishi na UKIMWI ili kuwaletea maendeleo huku akisisitiza kuwa Mkoa wake utaendelea kutekeleza mikakati iliyojiwekea ya kuinua maisha ya wanainchi wake ikiwa ni pamoja na mkakati wa kuwavusha salama mama na mtoto.

Aidha ameweka msimamo wake wa kutokuonesha nia yeyote ya kuomba ridhaa ya kugombea Ubunge katika uchaguzi wa mwaka huu huku akiwaonya watu ambao wamekuwa wakianza kudanganya kuwa atagombea ambapo alisisitiza kuwa nafasi hiyo ya ukuu wa Mkoa aliyopewa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli ni ya heshima kubwa.

“Naomba niliseme hili, na tayari nimeshalisema mara kadhaa hata hivi karibuni nilipokuwa nyumbani kwangu, kijijini Matufa, Babati Manyara nilipo hudhuria mazishi ya mtoto wa Kaka yangu aliyefariki kwa ajali ya Pikipiki kwamba nilikwenda kuungana na familia yangu katika msiba wa kijana wetu na si vinginevyo. Ninaridhika sana na nafasi hii niliyo nayo ya ukuu wa Mkoa” alisema Dkt. Nchimbi huku akishangiliwa na umati wa wadau wa mafunzo hayo

Baadhi ya waombolezaji wamesikika kupongeza msimamo wa kiongozi huyo, huku wakisema kuwa Msimamo huo unapaswa kuigwa na viongozi wengine kwa kuwa umejikita katika kuwaletea maendeleo wananchi badala ya kuwa na tamaa za madaraka. 

“Binafsi nampongeza sana Mama Nchimbi kwani kwa muda wote amekuwa aking’ang’ana na kuwaunganisha watu wote bila kujali dini wala rangi kwa, hata sisi leo ametutia moyo sana kiasi kwamba baada ya kutoka hapa tumekuwa na nguvu mpya ya kuchapa kazi na kushirikiana na Serikali yetu ya kujiletea maendeleo Zaidi ili tutoke katika nchi za uchumi wa kati na kwenda katika nchi tajiri duniani na tuna imani kubwa chini ya Rais wetu Magufuli tutafika” amesema Amina Huredi ambaye ni Mshiriki wa mafunzo hayo kutoka Singida

Mkurugenzi wa Utatifi wa NACOPHA Pantaleo Shoki amemshukuru Mkuu wa Mkoa na kumhakikishia kuwa wataendelea kushikiana na Serikali ili kuhakikisha kuwa malengo ya Mradi huo yanatimia kama yalivyopangwa.

Shoki amesema Mradi unalenga kufikia Mkakati wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupambana na UKIMWI(UNAIDS) wa 95-95-95 yaani asilimia 95 ya watu wote wanaoishi na maambukizi ya VVU wawe wamepima na kugundua afya zao,asilimia 95 ya watu wote waliopimwa na kukutwa na maambukizi wawe wameanza tiba na asilimia 95 walio kwenye tiba wawe wamefubaza virusi hivyo ifikapo 2030

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...