Muonekano wa jengo la Mkuu wa Wilaya kwa sasa Mara baada ya ukarabati.
 Katibu tawala Wilaya ya Kwimba akionyesha sehemu ya ofisi ya DC iliyokarabatiwa.

 Katibu Tawala Wilaya ya Kwimba Nyakia Chilukile akizungumza na waandishi wa habari mbele ya ofisi ya mkuu wa wilaya ambayo inakarabatiwa kwa sasa.

Na Mwandishi Wetu, Kwimba

Jumla ya fedha kiasi cha shilingi Milioni 70 zimetumika kukarabati ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza kati ya Milioni 105 zilizoombwa serikalini kupitia Force akaunti.

Hayo yameelezwa na Katibu tawala wa Wilaya Kwimba Nyakia Ally Chilukile Wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu  miradi mbalimbali iliyofanywa na Rais Dkt .John Magufuli Kupitia Force Akaunti.

Nyakia amesema Kuwa jengo hilo ambalo lilikuwa limechakaa na kupoteza muonekano limekamilika kwa asilimia90 mpaka sasa.

"Mimi Binafsi napenda kumpongeza Rais kwa maoni yake kwani imekuwa inakuja fedha ndogo lakini inafanya kitu kinaonekana "anasema Nyakia


Anasema kuwa mbali na ofisi ya Mkuu wa Wilaya pia wameweza kukarabati makazi ya Mkuu wa Ambayo yanajengwa kisasa zaidi kuliko ilivyokuwa hapo a wali.

Anataja kuwa katika fedha hizo mpaka sasa wamekwisha pokea kiasi cha fedha Milioni 70 kwa ajili ya ukarabati ofisi ya Mkuu wa Wilaya na kiasi cha milioni 60 kwa ajili ya ukarabati wa jengo la makazi ya DC.

Anaweka wazi licha ya kuomba fedha zaidi ya milioni 105 za ukarabati lakini no milioni 70 tu zimetumika kukarabati hivyo fedha zitakazo ongezeka zitatumika kwa ajili ya kununua Samani za ofisini na vitendea Nazi kama kompyuta na vitu vingine.

Kwa upande wake afisa tarafa wa Wilaya ya Kwimba Hamza Hamza amesema kuwa mradi huo ulianza mwezi may mwaka huu hivyo umetumia miezi miwili tu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...