Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akisisitiza jambo wakati wa mazunguzo na daadhi Wananchi waliojitokeza wakati wa ziara

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amefanya ziara katika eneo la mpaka wa Mkenda uliopo Wilaya ya Songea Vijijini Mkoani Ruvuma unaoinguanisha Tanzania na nchi Jirani ya Msumbiji. Ziara hii inalenga kibaini na kutatua changamoto mbalimbali ili kukuza biashara na uhusiano wa kidiplomasia baina ya Tanzania na nchi jirani ya Msumbiji. Katika ziara hiyo Dkt. Ndumbaro aliambatana na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi ya Wilaya ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Songea Mjini Mhe. Pololet Mgema.

Akiwa mpakani hapo Dkt. Ndumbaro amefanya mazungumzo na watumishi wa Idara mbalimbali za Serikali walipo katika ofisi za mpaka huo kwa lengo la kusikiliza changamoto na mapendekezo yanayolenga kuboresha namna ya utoaji huduma kwa wakazi wa eneo la mpaka na watumiaji wa mpaka huo. Aidha, Dkt. Ndumbaro pamoja na kutoa ufumbuzi wa baadhi ya changamoto, na kuahidi kuzifanyia kazi changamoto zilizosalia amewataka watumishi kuendelea kufanya kazi kwa ubunifu, jitihada na uaminifu.

Dkt. Ndumbaro pia ametembelea Ofisi za mpakani kwa upande wa Nchi jirani ya Msumbiji na kufanya mazungumzo na Watumishi walipo katika Ofisi hizo.

Mheshimiwa Ndumbaro, amewaleza wakazi na watumishi walipo mpakani humo kuwa Serikali inanendelea na hatua za kuzitatua changamoto kubwa zinazo changia ugumu wa utekelezaji wa majukumu ya kilasiku na kuadhiri mwenendo wa biashara mpakani hapo, ikiwemo ukosefu wa umeme, huduma ya mawasiliano na barabara ya kiwango cha lami.

Dkt. Ndumbaro amewapongeza Watumishi walipo mpakani kwa kazi nzuri wanayoifanya na amewahimiza Watumishi hao kuendelea kutekeleza Dilomasia ya Uchumi, kuendeleza uhusiano mwema na kushughulikia suala la Diaspora

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akisaini kitabu cha Wageni alipotembelea Ofisi ya Uhamiaji katika mpaka wa Mkenda uliopo Wilaya ya Songea Vijijini, Mkoani Ruvuma 




Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza na Wafanyakaozi wanahudumu katika mpaka wa Mkenda. Kushoto ni Mhe. Pololet Mgema Mkuu wa Wilaya ya Songea Vijijini.



Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro na Mkuu wa Wilaya ya Songea Vijijini Mhe. Pololet Mgema wakiwa katika picha ya pamoja baadhi ya wakazi wa mpakani Mkenda



Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akipokelewa na Maafisa Uhamiaji wa upande wa Msumbiji alipotembelea ofisi za mpakani Mkenda za nchi hiyo wakati wa ziara.



Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akisaini kitabu cha Wageni alipotembelea Ofisi ya Uhamiaji za Msumbiji zilizopo mpakani Mkenda, Ruvuma



Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro na Mkuu wa Wilaya ya Songea Vijijini Mhe. Pololet Mgema wakiwa katika picha ya pamoja baadhi ya Watumishi wa Mpakani kutoka Tanzania na Msumbiji
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akiendelea na ziara katika maeneo mbalimbali ya mpaka

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...