Na. Samwel Mtuwa - DSM.

Leo tarehe 7/7/2020 ambayo ni sikukuu ya Sabasaba Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) inayoshirika katika maonesho hayo imewavutia wageni wengi kufika katika Banda hilo wakiwa na hamu ya kuona na kushika  Madini mbalimbali yanayopatikana Tanzania  kama vile Tanzanite , Dhahabu, Zamaradi, Ganeti ya Nyekundu, Tomalini ya Pinki, Ganeti ya Kijani , pamoja na Madini ya  Akwamarini yaliyopo ndani ya Banda hilo.

Sambamba na Madini hayo , kivutio kingine ni mti uliogeuka kuwa Mwamba (Petrified Wood), kutokana na vivutio hivi vya kijiolojia wageni wote wanaofika katika Banda hili wanapata maelezo ya kina kutoka kwa wataalam juu ya maendeleo ya Utafiti wa Madini na Miamba unaofanywa na GST tangu ilipoanzishwa Mwaka 1925.

Maonesho haya yalizinduliwa rasmi tarehe 3/7/2020 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , mapema baada ya kuzinduliwa GST imepata fursa ya kutembelewa wageni wengine ambao ni;  Profesa Justinian Ikingura ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya GST , Mtendaji Mkuu wa GST Daktari Mussa Budeba , pamoja na Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu wa Serikali ya awamu ya Nne Mama Tunu Pinda.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...