Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema ongezeko la asilimia 34 ya mapato ndani ya nchi yanayokusanywa yanatokana matumizi ya Stempu za kodi za Kieletroniki (ETS) Kwenye bidhaa mbalimmbali.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (DIFT) Naibu Kamishna Mkuu wa TRA Msafiri Mbibo amesema kuwa matumizi ya stempu za kodi zilizowekwa na TRA zimechangia ongezeko la kodi kwa asilimia 34.

Mbibo amesema, stempu hizo zimewekwa katika bidhaa mbalimbali kama vinywaji vikali na sigara na tayari TRA imeanza mchakato wa kuweka kwenyw Vinywaji baridi ikiwemo Soda, Juisi na maji.

Amesema, awamu ya kwanza ya stempu hizo ilianza mwaka 2018 na matokeo yake yamekuwa chanya na wapo kwenye maandalizi ya awamu ya pili.

Ameeleza kuwa, viwanda mbalimbali vinavyotengeneza vinywaji baridi vimeshafunga mitambo ya kuwekea stempu hizo na lengo likiwa ni kudhibiti upotevu wa mapato na bidhaa feki mtaani.

"Baada ya kuweka stempu hizo ilisaidia kuondoa bidhaa feki mtaani na serikali kupata mapato yanayostahili," amesema.

Aidha, serikali inaendelea kutoa mafunzo kwa wamilili wa Viwanda wa vinywaji baridi namna ya kuweka stempu hizo na serikali inaendelea kutafuta njia rafiki ya ukusanyaji mapato kwa wananchi.

Mbibo ameongezea kuwa, TRA haikupata athari kubwa za ukusanyaji mapato kipindi cha janga la Virusi vya Corona kwani nchi iliendelea na shughuli za kimaendeleo kama kawaida na kutokufunga mipaka kama nchi zingine walivyofunga.

Mbali na hilo,TRA imewaomba wananchi kujitokeza kwenye banda lao na kupata huduma mbalimbali zinazotolewa ikiwemo ulipiaji wa leseni,kodi na malipo mengine ya serikali.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) akifafanua jambo wakati Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo Bw. Msafiri Mbibo (wa pili kulia) alipotembelea Banda la TRA kwenye Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SabaSaba).



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...