Katika Kuhakikisha kuwa Tanzania ya Viwanda inafikiwa ifikapo Mwaka 2021, Wakala wa Nishati Vijijini REA imedhamiria Kuwa Kila Kijiji Kitafikiwa na huduma za Umeme, ili kuendana na Kasi ya Uzalishaji Kupitia Nishati ya Umeme. 
 Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar es Salaam na Kaimu Meneja Mipango, Miradi na Utafiti , Mhandisi JENSEN MAHAVILE, wakati wa Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa Saba Saba.

Mhandisi MAHAVILE amesema Mpango huo Unawezekana Kwa Sababu ya Serikali Chini ya Rais Dkt JOHN MAGUFULI, Kutoa Kipaumbele Kwenye Miradi inayohusu Umeme Vijijini Kwa Kuhakikisha Kila Mwaka Bajeti inaongezeka.
Amesema Kupitia Miradi ya Usambazaji Umeme Vijijini inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijni REA, Kinachofanyika hivi sasa ni Kuupeleka Umeme hadi Kwenye Ngazi ya Vitongoji na Maeneo ambayo hayajafikiwa na Huduma ya Umeme.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...