Na Said Mwishehe,Michuzi TV

HATUTAKI Mazoea! Ndivyo ambavyo baadhi ya mashabiki na wapenzi wa timu ya soka ya Simba walivyokuwa wakishangilia baada ya kuibuka na ushindi wa bao 4-1 dhidi ya timu ya Yanga.

Simba na Yanga wamekutana leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na baada ya dakika 90 za mchezo wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Simba wameibuka na ushindi mnono na hivyo kuingia hatua ya fainali ya michuano hiyo.

Wakati mchezo huo uliokuwa na ufundi mwingi wa kusakata kabumbu kwa timu zote mbili , Simba walifanikiwa kupata bao la kwanza kupitia kwa mchezaji wake Fraga katika dakika ya 21.

Hivyo hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza kinamalizika Simba walikuwa wakiongoza kwa bao 1-0 dhidi ya timu ya Yanga.

Wakati wa kipindi cha pili kila timu ilionekana kurejea uwanjani wakiwa na kasi zaidi kiasi cha kuufanya mchezo huo kuwa wenye buradani ya soka ya kila aina.

Hata hivyo ilipofika dakika ya 50 ya mchezo huo Simba walipata bao la pili kupitia kwa mshambuliaji wake machachari Cleotus Chota Chama na dakika ya 52 Simba ikapata bao la tatu kupitia Luis Miquissone aliyekuwa kwenye ubora wa hali ya juu.

Hata hivyo kikosi cha Yanga nacho kiliamua kuongeza mashambulizi na kushambulia kwa kasi na ilipofika dakika ya 70 walipata bao la kwanza kupitia kwa mchezaji wake Faisal Salum a.k.a Fei Toto baada ya kuachia mkwaju mkali uliomshinda mlinda mlango Aishi Salum Manula.

Katika vuta nikuvute za mchezo huo Simba walionekana kuutawala mpira walifanikiwa kupata bao la nne kupitia kwa mchezaji wake Muzamiru Yassin.

Hivyo hadi dakika 90 za mchezo huo zinamalizika, Simba waliibuka na ushindi mnono wa bao 4-1.

Hata hivyo mashabiki na wapenzi wa Simba walionekana kuwa na furaha kutokana na ushindi huo kwa kuzingatia timu hizo zilipokutana kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara ,Yanga waliibuka na ushindi wa bao 1-0.Bao la Yanga lilifungwa na Bernard Morrison ambalo lilipachikwa jina na Waziri wa Fedha Dk.Philip Mpango ni bao la Mkuki wa sumu.

Hivyo Simba kuibuka na ushindi mnono kwenye mchezo wa leo wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho limerejesha heshima yao na sasa wanajiandaa kucheza fainali ya michuano hiyo dhidi ya Namungo FC.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...