* Ni kijiji ambacho hupata vifo 40 pekee kwa mwaka
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
NCHINI Italia, kijiji cha Alpine huko Locana kina uhaba wa watu licha ya kuwa na huduma zote muhimu ambazo nyingi zimefungwa kutokana na uhaba wa watu, hali iliyopelekea Serikali kupitia Meya wa Mji wa Locana, Giovanni Bruno kutangaza kuwa wanahitaji watu watakaohamia na kuweka makazi ya kudumu sambamba na kuzaliana katika kijiji hicho kwa dau la zaidi ya shilingi milioni 20.
Meya wa kijiji hicho amesema kuwa kijiji hicho kinapatikana kilometa 45 kutoka Mji wa Piedmont, Turin na kueleza kuwa kwa uchumi walionao wanategemea kuwahudumia wakazi wote watakaohamia eneo hilo katika huduma za nyumba, maduka, baa, shule pamoja na migahawa ambayo kwa sasa imefungwa.
Ameeleza kuwa watu wengi wameondoka hapo na kwenda kutafuta kazi hali iliyosababisha hata idadi ya wanafunzi kupungua jambo ambalo kama Meya hataki kusikia.
Ameeleza kuwa Locana ni kiini cha cha kivutio cha utalii cha Gran Paradiso na kwa sasa wanatafuta vijana wenye ujuzi kuanza shughuli zao hapo kwa kuwa maduka, baa na migahawa mingi imefungwa.
Aidha amesema kuwa eneo hilo ni zuri kwa kuwa lina maua, milima, sehemu za kuogelea, kupanda milima na sehemu za uvuvi.
Imeelezwa kuwa watu katika eneo hilo wamepungua kutoka watu 7000 katika miaka ya 1990 hadi kufikia watu 1500 na hiyo ni baada ya idadi kubwa ya watu kuhamia Turin kutafuta kazi.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...