Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV

MWENYEKITI wa Chama cha ACT Wazalendo Maalim Seif Sharif Hamad amekamilisha ziara yake  ya kichama iliyoanza Juni 29,2020 Kisiwani Pemba.

Ziara hiyo  mbali na shughuli nyengine za kuangalia uhai wa chama kiongozi huyo alikuwa na jukumu ya kuzibadilisha kamati za uongozi za majimbo na mikoa kuwa kamati maalum za ushindi kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, 2020.

Taarifa iliyotolewa leo Julai 15,2020 kwa vyombo vya habari na  Ofisa Habari Uenezi,Mahusiano na Umma wa ACT Wazalendo Abeid Khamis Bakari imesema kuwa kabla ya kukamilisha ziara yake katika mkoa wa Mjini Unguja kichama, Maalim Seif mapema leo asubuhi amerudisha fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea nafasi ya Uraisi wa Zanzibar kupitia chama hicho.

Ambapo Maalim ameweka wazi kwamba kwa upande wa Zanzibar chama kimejiimarisha sana na wanaomba kwa hamu kubwa uchaguzi ufike.

“Nimerudisha fomu ya kuomba ridhaa ya kuwa mgombea Uraisi kupitia chama changu cha ACT Wazalendo, na kama chetu kitanipitisha kuwa mgombea basi nasema wazi CCM Zanzibar wajiandae na anguko kubwa la fedheha,kwa uimara huu wa chama chetu, CCM Zanzibar tutawashida mara nne zaidi ya kura tulizowashinda mwaka 2015.

Baada ya mchakato huo Maalim Seif amekutana na kufanya kikao cha ndani na viongozi wa Matawi,Majimbo na Mkoa pamoja na Ngome za chama wa mkoa wa Mjini Unguja kwaajili ya kukamilisha ziara yake kikao kilichofanyika Vuga mjini Unguja.

Akizungumza na Viongozi wa mkoa wa Mjini, Maalim amewasisitiza wahakikishe wanachama wenyesifa wakiwemo Wanawake na Vijana wanajitokeza kwa wingi kugombea nafasi za Udiwani,Uwakilishi,Ubunge,Urais wa Zanzibar pamoja na Urais wa Jamuhuri ya Muungano kwani Chama cha ACT Wazalendo ni chama cha Kidemokrasia na mambo yoye yatakwenda kwa uhuru na uwazi mkubwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...