*Vyuo vya VETA na wanatengeneza bidhaa bora

Na Chalila Kibuda-Michuzi Globu.

MWENYEKITI  wa Bodi ya Mamlaka ya  Elimu ya Mafunzo Stadi (VETA), Peter Maduki, ameutaka uongozi wa VETA kuwafuatilia na kuwaunganisha wanafunzi waliotengeneza na kubuni bidhaa mbalimbali kutoka vyuoni.

Maduki aliyasema hayo jana wakati alipotembela banda la VETA  katika maonesho ya 44 ya biashara  ya kimataifa ‘sabasaba’  yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Amesema vijana wamekuwa wakibuni wa kuzalisha bidhaa mbalimbali zenye ubora na imara na zinazouzika kwenye soko la nchi na kufikia adhima ya serikali ya viwanda na rasilimali yenye ujuzi.

“Niwatake uongozi wa VETA kuwaunganisha wabunifu mfano waliotengeneza pikipiki  na viwanda ambavyo vinazalisha pikipiki hapa pamoja na wale wanaounganisha pikipiki nchini,”amesema

Amesema wazalishaji wa VETA wanazingatia ubora huku akibainisha kuwa wapo wenye mtazamo wa kudhani vitu vya nje ya nchi ndivyo vyenye ubora wakati wao vijana wazawa wanazalisha bidhaa zenye bora na wakati mwingine zile za nje zinakuwa hazina ubora.

“Vitu vinavyozalishwa VETA nimeviona vina ubora kuliko hata tunavyovifikiria kutoka nje, ubora huu unapatikana kutokana na malighafi zinazopatikana nchini"amesema Maduki.

Amesema kupitia maonesho hayo ameweza kuona bunifu mbalimbali zinazofanywa na vijana waliopo vyuoni na hata waliohitimu masomo yao.

 “Mafunzo haya wanayoyapata na kuyatumia yanaweza kusaidia kuchangia kuanzisha avaiwanda na akuviimarisha, kukuza ajira kwa vijana wanaomaliza katika vyuo mbalimbali,”alisema.

Aliongeza kuwa mafunzo hayo si tu  yanatoa ajira bali huwasaidia hata wale walio katika maeneo yao ya kazi kama kwenye kilimo na ufugaji ambapo wanaweza kujifunza kwa muda mfupi na kuongeza tija katika maeneo yao.

“Haya ni mambo makubwa , niwahimize wananchi ,walezi na wazazi waweze kuwatuma vijana wao kujiunga katika vyuo vyetu vya mafunzo ya ufundi stadi,”alisema.

Alitoa ombi kwa waajiri kutumia wanafunzi wanaotoka katika vyuo hivyo kuwaajiri kwani wanakuwa mahiri katika kazi zao na kushiriki kwenye uzalishaji moja kwa moja.

Maduki alitoa wito kwa vijana wanaomaliza mafunzo, kuanzisha shughuli zao binafsi kama ufundi seremala kwa kuzalisha bidhaa zao na kuuza.

“Nimefurahishwa  sana na maonesho ya mwaka huu kwasababu yameonesha picha hali ya uzalishaji wa bidhaa mbalimbali kutoka vyuoni" amesema.

Mwenyekiti wa Bodi ya VETA Peter Maduki akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea Banda la VETA katika Maonesho ya 44 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...