MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu mafundi umeme wawili na mmiliki wa nyumba mmoja, kutumikia kifungo cha miaka 12 jela na kulipa faini ya Sh.milioni mbili baada ya kupatikana na hatia ya kuingilia miundombinu ya umeme.
Washitakiwa hao ni Jiddah Abdallah, na Abel Myonga ambao ni mafundi umeme na Hashim Rwambo ambaye ni mwenye nyumba aliyeunganishiwa umeme wamehukumiwa kifungo hicho bila ya wao kuwepo mahakamani.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate amesema upande wa mashtaka kupitia mashahidi wake watatu waliweza waliofika mahakamani hapo kutoa ushahidi dhidinya washtakiwa wameweza kuthibitisha mashtaka pasipo kuacha shtaka mahakamani hapo na mashahidi watatu walitoa ushahidi kuthibitisha mashitaka hayo na washtakiwa ndio waliotenda kosa hilo.
Amesema, washtakiwa hao hawakuonekana tena mahakamani tokea ushahidi ulipomalizika kutolewa na juhudi za kuwapata wadhamini zilishindikana hivyo, mahakama ilitoa hukumu pasipo kuwepo washitakiwa.
"Mahakama inawatia hatiani washitakiwa wote na kuwapa adhabu mshitakiwa wa kwanza na wapili kutumikia kifungo cha miaka 12 jela na mshitakiwa wa tatu anatakiwa kulipa fidia ya Sh. milioni mbili na adhabu zao zitaanza pindi watakapopatikana," amesema Hakimu Kabate.
Kabla ya kutolewa kwa adhabu, Wakili wa Serikali Janeth Magoho aliomba Mahakama kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa ili iwe fundisho kwa wengine.
Inadaiwa katika tarehe isiyofahamika Agosti 2016 maeneo ya Mbezi Juu Goba kwa Sanya wilayani Kinondoni washitakiwa hao waliingilia miundombinu ya umeme kwa kumuunganishia umeme Rwambo.
Alidai tarehe hiyo hiyo waliharibu miundombinu kwa kuunganisha umeme iliyokuwa ikitoa huduma muhimu. Alidai kuisababishia mamlaka hasara ya Shilingi 2,114,228.26 kwa makusudi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...