MWANADADA Radhia Japhet Solomon mwenye Mapacha wanne, leo asubuhi amejitokeza kuchukua fomu ya kuwania ubunge wa. Viti maalum Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Kinondoni.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa UWT Mkoa wa Dar es Salaam, Grace Haule  idadi kubwa ya wagombea wa nafasi mbalimbali wamejitokeza kuunga mkono juhudi za Rais Dk. John Magufuli anayefanikisha maendeleo makubwa kwa nchi yetu.
Haule alisema hadi anachukua fomu Razia wagombea zaidi ya 180 wamejitokeza kuwania nafasi mbalimbali za UWT.
Alitumia fursa hiyo kueleza kwamba muitikio huo mkubwa wa wagombea Wanawake ni kazi ya hamasa waliyoifanya kuanzia ngazi ya matawi, Kata, Wilaya, Mkoa na Taifa.
Naye Radhia alisema amejitokeza kuwania nafasi hiyo baada ya kujipima kwamba anaweza.
  MWANADADA Radhia Japhet Solomon mwenye Mapacha wanne akiongea na wanahabari
 MWANADADA Radhia Japhet Solomon mwenye Mapacha wanne akikamilisha taratibu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...