Kila biashara hukuwa na kubadilika, hii ni sambamba na Benki ya Stanbic Tanzania ambayo imekuwa katika safari ya ukuaji unaoletwa na maendeleo ya wateja wake na watanzania kwa ujumla. Jambo ambalo limeipa benki hiyo motisha ya kubadilisha na kuunda kauli mbiu ambayo inafanania nafasi yake katika jamii.

“Wateja wetu mara nyingi hujiuliza kama ndoto zao zinaweza kutimia. Mfano; Je, ninaweza kumiliki nyumba ya ndoto yangu? Je, ninaweza kuwa na utajiri wa kutosha ili kutimiza mahitaji ya watoto wangu? 
 
Je, ninaweza kuibadili biashara yangu kuwa ya kimataifa? Hivyo kama mshirika wa kifedha, ni wajibu wetu kujibu maswali hayo. Na tunafanya hivyo kwa furaha kupitia kauli mbiu yetu mpya inayosema, ‘Inawezekana.” alisema Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo, Kevin Wingfield.

Aliongeza kuwa ‘Inawezekana’ ni kauli inayoakisi namna benki hiyo imekua, na jinsi inaendelea kufanya hivyo, kutokana na wanavyo hudumia wateja wao, na mtazamo walionao kwa Tanzania na fursa zilizopo nchini.

“Benki ya Stanbic inaamini kuwa ndoto ni chachu ya maendeleo. Hivyo ni lazima sisi na wateja wetu tuwe tayari kuchukua hatua mpya kufanikisha ndoto hizo.” alisema Wingfield. Wakati tunaunda kauli mbiu hii, tafiti zilionyesha kwamba watu pamoja na biashara zao, hutafuta mtoa huduma ambaye anawaamini na anawahamaisha. Yaani wanahitaji benki itakayowawezesha kufikia malengo yao – binafsi na kibiashara na ambayo itawathamini katika kila jambo. Kauli mbiu ya ‘Inawezekana’ inatupa fursa ya kufanya hivyo.” Alisema Wingfield.

Mwelekeo huu mpya ni kwaajili ya kuhamasisha imani juu ya Tanzania ya kesho huku tukionyesha ubunifu wa suluhu ambazo zinalenga kutoa huduma fanisi kwa wateja wetu. Vile vile unajumuisha jitihada nyingi zilizofanywa na benki ya Stanbic ili kuhakikisha wateja wake wanapata suluhu katika kipindi hiki chenye changamoto ya ugonjwa wa COVID-19.

Mfano mwezi Aprili, benki ya Stanbic ilitoa afueni ya ulipaji wa mikopo kwa muda wa miezi 3 hadi 6 kwa wateja wake ambao walishindwa kutimiza wajibu huo kutokana na madhara ya kibiashara yaliyotokana na mlipuko wa ugonjwa huo. Vile vile, benki ilianzisha shindano la ujasiriamali ambalo lililenga kutoa zawadi ya shilingi milioni 50 kwa biashara zilizoonekana kuwa bora zaidi ili kustahimili athari za COVID-19. Zaidi ya hayo, benki ilizindua Africa China Agency Proposition ambayo inasaidia makampuni kufanikisha shughuli zao za kibiashara na China.

“Lakini Sasa ni wakati wa kuwa na simulizi zenye matumaini, imani na mtazamo chanya. Kauli mbiu ya ‘Inawezekana’ ni chachu juu ya kutimiza ndoto zetu. Tunaamini kwamba huu ndio wakati sahihi kutambulisha kauli mbiu yetu hii ambayo inatupa hamasa kutimiza ndoto,’ alimaliza Wingfield. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...