Na Bakari Madjeshi,  Michuzi TV

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Bernard Membe rasmi amechukua Fomu ya kuwania Urais wa Tanzania kupitia Chama cha ACT-Wazalendo.


Membe amechukua Fomu hiyo ya kuwania Urais katika Makao Makuu ya Chama hicho yaliyopo Magomeni jijini Dar es Salaam kufuatia ombi la Wanachama na Mwenyekiti,  Maalim Seif Sharif Hamad kumuomba kuwania nafasi hiyo.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa Fomu na Katibu Mkuu wa Chama, Ado Shaibu,  Membe amesema uchukuaji wa Fomu hiyo ni mwanzo wa harakati za kuwania urais nchini, amesema  atazungumza kwa kirefu zaidi siku ambayo atarudisha Fomu hiyo.

"ACT Wazalendo inakwenda chap chap chap! hatuwezi kuchelewa, nitatekeleza miongozo ya Fomu hii, na nitaijaza fomu hii vizuri sana kwenye nukta nitaweka nukta na kwenye herufi kubwa nitaweka kubwa, kwenye herufi ndogo nitaweka ndogo ili asipite mtu akasema sikujaza vizuri fomu hii. Nitatema cheche siku ambayo nitarudisha fomu hii,  hapa nina mzigo kweli kweli",  amesema Membe.

Membe amesema ameona jina lake la kwanza katika orodha ya wanaowania urais kupitia Chama hicho, lakini amesema anashukuru yeye kuwa wa kwanza kuchukua Fomu hiyo,  hata hivyo wengine wanaruhusiwa kutokana na Demokrasia.

"Nitaheshimu kila mnalolitaka na ndio maana sikutaka kabisa kuchelewesha kutoa majibu,  Wakubwa wako wanavyokwambia na kukuuliza swali! Swali limeulizwa leo limejibiwa",  amesema Membe.

Amesema anashukuru sana kwa kitendo cha Uongozi wa Chama, Wanachama wote kwa kumuunga mkono sambamba na Kiongozi wa Chama,  Zitto Kabwe na Mwenyekiti, Maalim Seif Sharif Hamad.
  Katibu mkuu ACT Wazalendo Ado Shaibu akimkabidhi Mhe Bernard Membe begi lenye fomu za kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho
 Mhe.Membe akiwaonesha Waandishi wa Habari (hawapo pichani),akiwaonesha begi lenye fomu za kuwania Urais mara baada ya kukabidhiwa.Picha na Michuzi JR -MICHUZI MEDIA.
 Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya nne,Mhe  Bernard Membe akizungumza na Waandishi wa Habari leo mara baada ya kuchukua fomu ya kuwania Urais wa Tanzania kupitia Chama cha ACT-Wazalendo. Membe amechukua Fomu hiyo ya kuwania Urais katika Makao Makuu ya Chama hicho yaliyopo Magomeni jijini Dar es Salaam kufuatia ombi la Wanachama na Mwenyekiti,  Maalim Seif Sharif Hamad kumuomba kuwania Urais.

Mhe. Membe alipokuwa akiwasili kwenye  ofisi za Makoa Makuu ya chama cha ACT Wazalendo zilizopo Magomeni,Kinondoni jijini Dar kuchukua Fomu  ya kuwania Urais  kufuatia ombi la Wanachama na Mwenyekiti,  Maalim Seif Sharif Hamad kumuomba kuwania Urais
  Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya nne,Mhe  Bernard Membe akisaini fomu ya kugombea Urais ndani ya chama hicho,kulia ni Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...