Na Amiri Kilagalila,Njombe

Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya YONO AUCTION MART LTD ambao ni mawakala wa kukusanya kodi ya Serikali Scolastika Cristian Kevela,kama kada wa Chama cha Mapinduzi amefika ofisi za chama hicho mkoa wa Njombe na kuchukuwa fomu ya ubunge viti maalumu mkoa wa Njombe.

Scolastika Kevela amesema ameona haja na nia kubwa ya kuwatumikia wananchi wa mkoa wa Njombe kwa kuwa muwakilishi wao kwa sasa hususana wanawake ili kufikia lengo na haja ya kutatua matatizo ya wanawake mkoani Njombe.

“Nimekuja Njombe kutimiza wajibu wangu wa kikatiba kama kada wa Chama cha Mapinduzi,nami sasa kama kada nimechukuwa fomu ya ubunge viti maalum mkoa wa Njombe” alisema Scolastika Cristian Kevela Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya YONO AUCTION MART LTD.

Aidha kutokana na utaratibu wa chama hicho amesema hawezi kuzungumza mambo mengi mpaka utaratibu mwingine wa chama utakapofika.
 Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya YONO AUCTION MART LTD ambao ni mawakala wa kukusanya kodi ya Serikali Scolastika  Cristian Kevela akizungumza kwa kifupi mara baada ya kuchukuwa fomu.
 Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya YONO AUCTION MART LTD ambao ni mawakala wa kukusanya kodi ya Serikali Scolastika  Cristian Kevela akisaini nakala ya wagombea waliofika na kuchukuwa fomu za wagombea ubunge wa viti maalum mkoa wa Njombe.
 Kushoto Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya YONO AUCTION MART LTD ambao ni mawakala wa kukusanya kodi ya Serikali Scolastika  Cristian Kevela,akionyesha fomu ya ubunge viti maalum mkoa wa Njombe mara baada ya kukabidhiwa na katibu wa chama hicho Merry Mkoka wa Kulia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...