Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) imefanya ukaguzi wa Magari ya taka eneo la Sayansi, Vingunguti na Kurasini wakiongozwa na Maofisa wa DAWASA na Wakaguzi wa Polisi ili kuona magari hayo kama yanakidhi vigezo na kupewa cheti ili kuondoa usumbufu kati yao na Jeshi la Polisi.

DAWASA inafanya ukaguzi wa Magari hayo lengo ikiwa ni kusajili na kutoaji vibali vya uendeshaji  kuanzia Julai 20, 2020 hadi August 4, 2020 sambamba na kuhakikisha kuwa Majitaka yanayonyonywa sehemu mbalimbali yanamwagwa kwenye mabwawa ya kutibu majitaka yanayomilikiwa na DAWASA.

Akizungumza wakati wa Ukaguzi wa Magari hayo, Afisa Biashara wa DAWASA, Daniel Mauna amesema zoezi hilo la kukagua ubora wa magari  ya majitaka ni muhimu ili kuhakikisha wanatoa vibali kwenye magari yaliyo mazima ili kuendana na kazi iliyopo.

Mauna amewataka wenye magari kwa kushirikiana na madereva wa magari ya majitaka kuyaleta magari hayo ili kukaguliwa na kuondoa kukamatwa na Askari wa Usalama barabarani. 

Mauna amesema vigezo vya ukaguzi wa Magari hayo ni lazima kuwa na Picha mbili za rangi za mmiliki wa gari na nakala ya kitambulisho chake (KURA, UTAIFA AU HATI YA KUSAFIRIA), Nakala ya kadi ya gari, nakala ya bima ya gari na nakala ya leseni ya udereva vilivyothibitishwa na Mwanasheria, Copy ya wakala wa vipimo (WMA) inayodhibitisha ujazo wa tanki na Hati ya ukaguzi kutoka Polisi (Vehicle Inspection Report).

 DAWASA imesesema baada ya muda wa usajili kuisha, yeyote atakayekutwa anatoa huduma ya unyonyaji na usafirishaji wa Majitaka katika eneo la huduma la DAWASA bila kibali hai cha uendeshaji atachukuliwa hatua kali za kisheria. Wananchi wanashauriwa kutumia Magari ya Majitaka yaliyosajiliwa na DAWASA. na Magari yatakayopata vibali yatabandikwa stika za DAWASA.


Kazi ya ukaguzi na utoaji vibali vya uendeshaji itafanyika eneo la Vingunguti bwawani na Shimo la udongo Kurasini. Gharama ya usajili ni Tsh 100,000/= (itakayolipwa kupitia control namba baada ya kukamilisha vigezo vyote vilivyowekwa.) Wasiliana nasi  huduma kwa wateja 0800110064 (BURE) 0735 202121(whatsap)  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano - DAWASA
 Afisa Biashara wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Paul Gabriel akitoa ufafanuzi kwa madereva wa magari ya kubeba Majitaka kuhusu namna ya  kushiriki katika ukaguzi wa magari yao katika eneo la Sayansi jijini Dar es Salaam 
 Afisa Biashara Afisa Biashara wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)  Daniel Mauna akizungumzia namna mamlaka hiyo ilivyojipanga kwa kushirikiana na askari wa usalama barabarani na wakaguzi wa magari kitengo cha polisi usalama barabarani ili kukagua magari ya Majitaka na kutoa vyeti bara baada kumalizika kwa ukaguzi huo.
Mkaguzi wa magari kitengo cha polisi usalama barabarani Gulen Mbwambo akikagua magari mbalimbali katika eneo la kumwaga Majitaka lililopo Vingungiti jijini  Dar es Salaam ili kuona magari yao kama yanakidhi vigezo na kupewa cheti ili wasisumbuliwe na polisi pamoja na kutambulika na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA).
Mkaguzi wa magari kitengo cha polisi usalama barabarani Gulen Mbwambo  akipata maelezo pamoja na kujaza fomu za ukaguzi wa magari ya Majitaka mara bada ya kukaguliwa ili kujua ubora wa magari hayo.

Afisa Biashara wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Paul Gabriel akitoa ufafanuzi kwa madereva wa magari ya kubeba maji taka kuhusu namna ya  kushiriki katika ukaguzi wa magari yao katika eneo la Vingungiti jijini  Dar es Salaam .


Afisa Biashara Afisa Biashara wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)  Daniel Mauna akichukua taarifa kwa mmoja wa madereva wa magari ya Majitaka mara baada ya kumaliza kukaguliwa kwa gari ilo wakati wa zoezi lililofanyika katika eneo la kumwaga Majitaka ya Vingunguti jijini Dar es Salaam.
Afisa Biashara wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Paul Gabriel akisisitiza jambo wakati wa zoezi la ukaguzi wa magari ya Majitaka katika  eneo la Vingunguti jijini Dar es Salaam 
Afisa Biashara Afisa Biashara wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)  Daniel Mauna akitoa ufafanuzi kwa deeva wa gari la Majitaka wakati wa zoezi la ukaguzi wa magari ya maji taka yaliyofika katika eneo la Vingunguti kwa ajili ya kumwaga maji katika eneo hilo leo jijini Dar es Salaam
Moja ya bwawala majitaka lililopo katika eneo la Vingunguti jijini  Dar es Salaam
Baadhi ya magari ya Majitaka yakimwaga maji hayo katika moja ya bwawa lililopo katika eneo la Vingunguzi wakati wa ukaguzi wa magari hayo yakiongozwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) wakishirikiana na wakaguzi wa magari kitengo cha polisi usalama barabarani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...