Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Mwanahabari Ally Thabit Mbungo  ametia nia ya kugombea nafasi ya udiwani kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) kata ya Kijichi.

Mbungo amekuwa mwanachama wa 16 kuchukua fomu kuwania nafasi hiyo ya udiwani.

Akizungumza na Michuzi Blog, Mbungo amesema hii sio mara ya kwanza kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo katika Kata ya Kijichi kwani alishachukua 2015.

Amesema, lengo kuu la kuwania nafasi hiyo ni kutaka kuondoa ile dhana ya kuwa mlemavu hawezi kuongoza au kushika nafasi ya juu.

"Nimechukua fomu hii, nataka niwaelimishe watu wenye ulemavu wasikae nyuma waje kuchukua fomu kwani maendeleo yanaletwa na mtu yoyote," amesema

Mbungo amesema, mbali na kutaka kuondoa dhana potofu ya walemavu pia anaunga mkono juhudi zinazofanywa na Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya ya kuleta maendeleo nchini.

Aidha, ameweka wazi kuwa hatakata tamaa iwapo kura zake hazitatosha tena kwa mwaka huu na atamuunga mkono mtu atakayepitishwa na Kamati ya Chama.

Katibu Mwenezi wa CCM Kata ya Kijichi Abdalla Limbanga amesema ni wanachama 16 tayari wameshachukua fomu ya kuwania nafasi ya udiwani akiwemo mwanahabari Mbungo.

Amesema, hii ni mara ya pili Mbungo anaonesha uthubutu ingawa ni mlemavu na hili linaonesha kuwa walemavu wanayo nafasi ya kuwa mwakilishi wa wananchi.

Mbungo ni mlemavu wa macho na ana taaluma ya uandishi wa habari akifanya kazi katika kituo cha Newala FM.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...