Na Woinde Shizza, KILIMANJARO

MWANAHARAKATI wa haki za wanawake hapa  kutoka Shirika la Haki za Wanawake Tanzania Joyce Kiria 'The Super woman' amewataka wanawake wote nchini Tanzania kuendelea kusimama imara katika kugombea nafasi mbali mbali za uongozi katika Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 25,2020.

Akizungumza na vyombo vya Habari mwanaharakati huyo amesema kuwa kwa muda wa miaka mitano ya  Rais Dk.John Magufuli kumekua na muamko mkubwa kwa wanawake kufanya kazi kwa bidii katika nafasi walizopewa bila kuwepo na utumbuaji .

Amesema kuwa wanawake wa ukanda wa Kaskazini wajitokeze kufanya mabadiliko katika kugombea nafasi mbalimbali kuanzia ngazi ya udiwani na ubunge kwa lengo la kushika nafasi na kusaidiana na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan katika kupambani haki na uwajibikaji wa mwanamke

"Namshukuru Rais kwa kututhamini na kutupa nafasi katika uongozi wake kutupa nafasi akiwemo mama Samia Suluhu ,Ummy mwalimu, mama Joyce Ndarichako pamoja na wanawake wengi walioko katika wizara mbalimbali ambao wote wanafanya vyema sana kusimamia haki za wanawake na maendeleo ya wa Tanzania kwa ujumla,"Kiria

Ameongeza kuwa mwaka huu wanawake wameshuhudia maboresho ya vituo vya afya pamoja zahanati na kupungua matukio makubwa ya kina Mama kujifungulia njiani na kupata uduma za kitabibu kuanzia kata mpaka hospital za rufaa jambo ambalo limesaidia kupungua vifo vya Mama na mtoto

Amefafanua licha ya Serikali ya awamu ya tano kutoa kipaumbele kwa wanawake kushika nafasi za kuu serikalini pia wanawake kwa sasa wanajitambua na kujituma haaa katika kujiendeleza kielimu na kutatua changamoto za kifamilia

Joyce Kiria ambaye pia amekuwa mstari wa mbele kufuatilia na kutatua changamoto zinazowapata wanawake amesisitiza umuhimu wa wanawake kuamka na kuamini wanaweza kuleta mabadiliko,hivyo kikubwa ni kuhakikisha wanajitokeza na kuomba nafasi katika uchaguzi mkuu mwaka huu.
Picha Mwanaharakati wa haki za wanawake hapa nchini Joyce Kiria 'The Super woman', kutoka Shirika la haki za wanawake Tanzania  akizungumza  na Waandishi wa habari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...