Na Chalila Kibuda,Michuzi TV

Mwenyekiti wa  wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Kisukulu  Shaban Uronu  amechukua fomu ya   ya kugombea ubunge katika Jimbo la Segerea.

Akizungumza na Mwandishi wa Michuzi Michuzi TV Mwenyekiti  huyo amesema amefikia uamuzi huo ili kuweza kusukuma gurudumj la maendeleo kwa  wanasegerea pale tu atakapoteuliwa katika chama.

Amesema kuwa anachosubiri ni katika mchakato ndani ya chama akipita hapo ni kuipepelusha bendera ya chama hicho.Amesema uwezo anao wa kupeperusha bendera hiyo kutokana na kuwa karibu na wananchi wa Jimbo hilo.

Aidha amesema kuwa kazi ni kuendeleza mazuri zaidi kutokana na sera za Rais Dkt.John Pombe Magufuli ya kuwainua wanyonge.Uronu  amesema Mbarali ikifanikiwa kupita itabadilika Sana kutokana na michango yake katika kuweza kutatua changamoto.

"Hapa ninachosubiri ni kuungwa mkono na wanachama wa Jimbo kunichagua kwa lengo moja ya kupigania maendeleo ya wanambarali na kauli mbiu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya kwenda kisasa zaidi  kuleta mabadiliko ya kiuchumi"amesema Uronu.

Hata hivyo  amesema kama kijana amekuwa na maono mengi ya kutaka vijana kuinuka kiuchumi katika kuwaunganisha kwenye vikundi.
 Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala Idd Mkoa (kushoto)akimkabidhi fomu ya kugombea ubunge wa Jimbo la Segerea  Mwenyekiti wa CCM kata ya Kisukulu Shaban Orunu katika ofisi za chama hicho Leo Ilala jijini Dar es Salaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...