Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson amekabidhi kadi ya shukrani kwa Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kwa niaba ya familia ya Baba Askofu Rabbi Mwakanani wa kanisa la The Evangelical Brotherhood Church.

Dkt.Tulia amekabidhi kadi hiyo ya shukrani jana katika ibada ya mazishi ya mke wa Askofu Rabbi katika Kanisa la Uinjilisti la Undugu Ushirika wa Wana wa Mungu Mbeya mjini na kupokelewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo, Dkt Godlove Mbwanji.

Kadi hiyo imetolewa ni utekelezaji wa maelekezo yaliyotolewa na Bi. Rhoda Mwakanani (Mke wa Askofu) alipokuwa akipatiwa matibabu katika hospitali hiyo hadi umauti ulipomkuta tarehe 2/7/2020.

Katika tukio hilo pia limeshuhudiwa na watu mbalimbali akiwemo Baba Askofu Rabbi Mwakanani mwenyewe na Katibu wa Afya wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya Bi. Myriam Msalale.
 Naibu Spika Dkt.Tulia Ackson akikabidhi kadi ya shukrani kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya  Rufaa ya Kanda Mbeya Dkt Godlove Mbwanji kwa niaba ya familia ya Baba Askofu Rabbi Mwakanani wa kanisa la The Evangelical Brotherhood Church (kushoto) anayeshuhudia ni Katibu wa Afya wa Hospitali hiyo, Bi. Myriam Msalale. Tukio lililofanyika jana Kanisa la Uinjilisti la Undugu Ushirika wa Wana wa Mungu Mbeya mjini.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...