Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Ajira na Vijana, Anthony Mavunde akiwa na fomu yake ya kuomba kuteuliwa kugombea Ubunge Jimbo la Dodoma Mjini baada ya kujitokeza Ofisi za CCM Wilaya kuchukua fomu hiyo.

Charles James, Globu ya jamii
NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana na Ajira, Anthony Mavunde amekua miongoni mwa watia nia waliochukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea Ubunge Jimbo la Dodoma Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi.

Mavunde amefika leo Ofisi za CCM Wilaya ya Dodoma Mjini na kukabidhiwa fomu hiyo ambapo amesema kama atapata nafasi ya kuwatumikia wananchi wa Dodoma kwa mara ya pili atahakikisha anaendelea palepale alipoishia.

Akizungumzia wingi wa wagombea waliotia nia Jimbo hilo ambao ni 47, Mavunde amesema hiyo ni ishara ya ukuaji wa Demokrasia ndani ya chama chao pamoja utendaji kazi wa Rais Magufuli kuwavutia walio wengi.

" Nimekua Mbunge wa Dodoma kwa miaka mitano, niseme tu pamoja na maendeleo makubwa ambayo jimbo letu imeyapata bado nilikua najifunza Ubunge, sasa niko tayari kuwatumikia wananchi wangu kwa miaka mitano mingine ili kuchochea zaidi maendeleo.

Niwashukuru sana wananchi wa Dodoma kwa kunipa nafasi ya kuwatumikia kwa miaka mitano na Leo nimekuja tena kuchukua fomu kuomba ridhaa kwa mara nyingine ya kuendelea kuwatumikia, niko tayari kuendelea kuwatumikia kwa nguvu, akili na moyo wangu wote," Amesema Mavunde.

Amesema dhamira yake ni kuendelea kuiletea heshima Dodoma kama ambavyo ndani ya miaka mitano Jiji hilo limepiga hatua kubwa za kimaendelea ikiwemo kuongoza kwa ukusanyaji wa mapato, kuongoza kwa mtandao wa barabara za lami pamoja na miradi mikubwa ya kimkakati.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...