Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV

MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi( CUF)Profesa Ibrahim Lipumba kwa kutumia Mamlaka ya Kikatiba,  amemsimamisha Naibu Katibu Mkuu Zanzibar  Faki Suleiman Khatib.

Taarifa ya CUF kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo Julai 4,2020 imesema hatua hiyo ni katika kutekeleza agizo la Baraza Kuu la kuondoa Mapungufu na Kuimarisha Kamati Tendaji.

Hivyo nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Zanzibar itajazwa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa linalotarajiwa kuketi mwishoni mwa mwezi huu.

Aidha Mwenyekiti amemteua  Nadhira Ali Haji kuwa Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Sheria kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Katibu Mkuu wa Chama, Haroub Mohammed Shamis.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo Prof.Lipumba ameyafanya hayo asubuhi ya leo huko Zanzibar akiwa kwenye ziara fupi ya kumtambulisha Katibu Mkuu Mpya na kushughulikia Maagizo aliyopewa na Baraza Kuu lililoketi wiki iliyopita Ukumbi wa Shaaban Khamis Mloo, Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...