*Wataka wadau wasifanye  kazi bila kusajiliwa na Bodi hiyo.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

BODI Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi nchini Tanzania (PSPTB), imezindua rasmi wimbo maalum wenye lengo la kuhamasisha shughuli mbalimbali zinazofanywa na bodi hiyo.

Akizindua wimbo huo jana jijini Dar es Salaam katika viwanja vya maonesho ya 44 ya biashara ya kimataifa maarufu kama sabasaba, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji  wa bodi hiyo, Godfred  Mbanyi alisema wimbo huo umeweka msisitizo katika suala la usajili ambao kwa mujibu wa sheria iliyoanzisha bodi hiyo wataalamu wote wa ununuzi na ugavi wanatakiwa wawe wamesajiliwa na bodi ndipo waweze kufanya kazi za ununuzi.

Alisema ni kosa la kisheria kwa mujibu wa kifungu cha 11cha sheria namba 23 ya mwaka 2007 iliyoanzisha bodi hiyo ni kosa kwa mtu yeyote kufanya kazi ya ununuzi na ugavi bila kusajiliwa na bodi."Wimbo huo utaweka msisitizo katika jambo hilo lakini pia utaelezea kazi mbalimbali za bodi kama kuwahimiza watu kuja kufanya mtihani ili waweze kuwa na sifa za juu za taaluma za ununuzi na ugavi," alisema

Aidha alisema katika wimbo huo umeweka kutangaza kazi za ushauri wanazozitoa na mafunzo mahususi ya taasisi za serikali na Binafsi ."Katika wimbo huo tumeelezea mafanikio tuliyopata na kuonyesha taasisi ambazo wameweza kuzitolea mafunzo yaliyowasaidia kufanya vizuri katika eneo la manunuzi," alisema

Alitoa wito kwa wataalamu waliopo vyuoni na makazini wajikite katika suala la usajili na wasisahau kupandishwa madaraja wasipofanya mitihani ya bodi ili waweze kupata sifa.Wimbo huo utasambazwa katika vyombo vya habari,vyuo vyao na kwenye mikutano yao ili kuongeza uelewa kwa wananchi juu ya kazi ya bodi hiyo.



 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Pstbt Godfred Mbanyi akiwa amebonyeza wimbo wa kuhamasisha  utoaji wa elimu kwa wadau mbalimbali kuhusiana na kazi za bodi hiyo.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji  PSTBT Godfred Mbanyi akizungumza na waandishi habari kuhusiana na bodi hiyo inavyofanya kazi pamoja na uzinduzi wa wimbo kuhamasisha wananchi kujua kazi za bodi katika maonesho ya biashara kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...