Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi),Dkt. Rashid Tamatamah akitoa ushauri kuhusu ufugaji wa samaki kwa kutumia matanki wakati alipotembelea banda la SUMA JKT kwenye maonesho ya 44 ya kimataifa ya Biashara yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalim  Nyerere jijini Dar es salaam
 Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi),Dk. Rashid Tamatamah, akipokea zawadi kutoka kwa Florence Mahimbo, wakati alipotembelea Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea kwenye viwanja vya  Mwl. Nyerere,  jijini Dar es salaam.
 Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), DKt. Rashid Tamatamah akipata maelezo kutoka kwa mtafiti wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo nchini (TALIRI), Bi.Neema Urassa, wakati alipotembelea maonesho ya 44 ya biashara ya kimataifa yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalim  Nyerere,  jijini Dar es salaam.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi-Uvuvi Dkt.Rashid Tamatamah akizungumza na waandishi wa habari mara baada yabkutembelea maonesho ya Biashara kimataifa yanayoyofanyika katika viwanja vya Mwalimu nyerere jijini Dar es Salaam.



Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Serikali imesema kuwa inatekeleza mradi wa matotolesho ya vifaranga vya samaki kupitia mradi wa usimamizi wa uvuvi wa kanda ya Kusini Magharibi mwa bahari ya Hindi (SwioFish), kwa lengo la kukidhi soko la mahitaji ya samaki hapa nchini pamoja  kuchochea uchumi wa viwanda.

Hayo ameyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi- Uvuvi Dkt. Rashid Tamatamah  wakati alipotembea   maonyesho ya Sabasaba, amesema, mradi huo utasaidia kuibua sekta ya uvuvi na viwanda na kutoa fursa ya wanafunzi kujifunza kwa vitendo na kuwa mahiri katika kuijua sekta hiyo ikiwa ni kusaidia wananchi katika ufugaji.

Amesema hivi sasa mradi huo unatekelezwa Kunduchi jijini Dar es Salaam  ambapo ujenzi huo utaanza Oktoba mwaka huu.

"Mradi kama huu utasaidia kukuza sekta ya viwanda na uvuvi na kutoa elimu kwa wanafunzi ambao watapata fursa ya kujifunza  kwa vitendo,"alisema Tamatamah.

Amesema tayari mchakato wa ujenzi wa maabara Kunduchi umeanza ambapo watashirikiana na chuo Kikuu cha Dar es Salam na baada ya miezi mitatu ujenzi utaanza.

Tamatamah alisema hapo awali tegemeo kubwa la samaki lilikuwa ni maji halisi lakini kwa sasa teknolojia za kisasa zimesaidia kupata samaki wengi kwa ajili ya mahitaji.

Hata hivyo alisema katika maonyesho ya mwaka huu watatumia  kutoa changamoto kwa wavuvi kwa kutoa elimu ya kuvua samaki wanaofaa kuliwa.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...