Walinzi nane wa Kampuni ya Ulinzi ya Security Group ya Afrika (SGA) Tanzania Ltd na wenzao 12 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo.
Walinzi wa nane wa Kampuni ya Ulinzi ya Security Group ya Afrika (SGA) Tanzania Ltd na wenzao 12 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  jijini Dar es Salaam leo.

WALINZI nane wa Kampuni ya Ulinzi ya Security Group ya Afrika (SGA) Tanzania Ltd na wenzao 12 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka matatu likiwemo shtaka la wizi na utakatishaji fedha wa  zaidi ya Sh bilioni mbili mali ya NMB benki.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na 
Wakili wa Serikali, Faraja Ngukah imewataja washtakiwa watano ambao ni ndugu kuwa ni Manjestus Mselema (44), Bernadetha (45) ambaye ni mama wa nyumbani na Mkazi wa Mbagala, Agnes  (29) Hotelia, Oswald Mselema (49) na Olaph Mselema (35)  ambapo wote ni walinzi.

Wengine ni Beda Mkali (51) ambaye ni CTI Control, Kais Nasibu (35), John Selestine (45), Edes Hyera (43), Engelbert Masare (45), Bernad Victor (39) na Sylidion Odil (42), Tulipo Mwamuzi (40) ambaye ni dereva, Grace Komba (32) Hotelia, Janeth Shilla (59) Wakala wa Kampuni ya Eternal International Ltd, Godwin (52) Fundi Mwashi na Anold Erio (25), Florah Mwita (25) mfanyabiashara na  Tispo Mwasakieni (27) maarufu Ronic Kinyozi na mkazi wa Kawe.

Akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Yusto Ruboroga, wakili Ngukah amedai, katika tarehe tofauti mwaka 2020, maeneo ya Dar es Salaam washitakiwa Manjestus, Mwakuzi, Godwin, Anold, Agnes, Mwita, Victor na Odil walikula njama ya kuongoza genge la uhalifu ili kufanya kosa la wizi.

Inadaiwa kuwa, Juni 8, 2020 huko maeneo ya Mbezi Beach wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam, washtakiwa waliiba Sh 2,082,000,000 mali ya NMB Benki

Katika shtaka la tatu imedaiwa Juni 8,2020 huko katika maeneo ya Mbezi Beach wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam, washitakiwa walijipatia Sh 2,082,000,000 mali ya NMB wakati wakijua kuwa fedha hizo ni zao la kosa tangulizi la wizi.

Washtakiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote kwa sababu mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na Hakimu Ruboroga ameahirisha kesi hiyo hadi Julai 28, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na washitakiwa wote wamerudishwa rumande kwa sababu mashitaka yanayowakabili hayana dhamana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...