Na Said Mwishehe,Michuzi TV.
MAKADA wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) katika Wilaya
ya Temeke jijini Dar es Salaam wamejitokeza kwa wingi kuanza kuchukua fomu za
kuwania nafasi za ubunge ambapo jimbo la Temeke waliochukua fomu ni 38 wakati
jimbo la Mbagala ni 41.
Akizungumza na Michuzi TV na Michuzi Blog leo
Julai 14,2020, Katibu wa Siasa na Uenezi wa Wilaya ya Temeke jijini Dar es
Salaam Ally Kamtande amesema kuwa katika Wilaya hiyo muamko wa wanaCCM kuchukua
fomu za kuwania nafasi za udiwani, ubunge , pamoja na viti maalum kwa nafasi ya
ubunge na udiwani imekuwa kubwa.
Amefafanua hadi jioni ya leo saa 10 jioni kwa
nafasi ya ubunge ambao wamechukua fomu kwa Jimbo la Mbagala imefikia 41 na
Temeke waliochukua fomu kuwania ubunge ni 38.
"Watia nia ambao wamechukua fomu za ubunge
kwa Mbagala ni 41 na kati ya hao Temeke ni 38 na kati hao 38 wanawake ni
wawili,"amesema Kamtande na kusisitiza kuwa baadhi ya watia nia
waliochukua fomu wawili wamesharudisha fomu za kuwania ubunge ambapo mmoja
anatoka Jimbo la Temeke na mwingine anatoka jimbo la Mbagala.
Hata hivyo ameendelea kusisitiza umuhimu wa
watia nia waliochukua fomu na wale ambao watajitokeza kuhakikisha wanazingatia
tararibu ambazo zimewekwa na Chama kwani kinyume na hapo watapoteza sifa.
"Tunawakumbusha watia nia wa nafasi zote
wawe makini katika kufuata sheria, kanuni na taratibu ambazo zimewekwa.Huu sio
wakati wa kampeni bali ni kipindi cha kuchukua na kurejesha fomu
tu,"amesema Kamtande na kusisitiza hawatajii kusikia kauli zinazoashiria
kuanza kampeni kabla ya wakati.
Kuhusu muamko watia nia kujitokeza kwa wingi
Kamtande amesema kuna sababu nyingi lakini uwazi ambao umeoneshwa kwenye ngazi
ya kitaifa ndani ya Chama hicho imekuwa chachu kubwa lakini pia utendaji kazi
uliotukuka kwa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa
Dk.John Magufuli.
Hata hivyo watia nia kadhaa wamepata fursa ya
kueleza sababu za kuchukua fomu za kuwania nafasi aidha kwenye udiwani au
ubunge huku wakieleza kuwa kwa kuwa muda wa kampeni bado hujafika kwa sasa ni
uchukuaji na urejeshaji fomu tu na baada ya hapo watakuwa na mengi ya kueleza
kwa wananchi.
Mtia nia wa nafasi ya udiwani wa Viti Maalum
Kata ya Makangalawe Rebecca Eliazar akipata maelekezo ya jinsi ya kujaza fomu
hiyo baada ya kuichukua leo Julai 14,2020 katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi
(CCM) Wilaya ya Temeke.
Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama
Cha Mapinduzi(UVCCM) Andrew Gwaje (kulia) akitoa maelekezo ya jinsi ya kujaza
fomu ya kuwania ubunge kwa mtia nia ya ubunge Jimbo la Temeke Adil Mohamed
jimbo
Mtia nia wa jimbo la Temeke jijini Dar es Salaam
Mwalim Kwame Kambulu(kushoto) akiwa amekabidhiwa fomu ya kuwania jimbo hilo la
Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM) Andrew
Gwaje(kulia).
Mtia nia wa nafasi ya Ubunge katika Jimbo la
Mbagala jijini Dar es Salaam Buluba Mabelele(kushoto) akikabidhiwa fomu ya
kuwania jimbo hilo kutoka kwa Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha
Mapinduzi(UVCCM) Andrew Gwaje(kulia).
Mtia nia wa nafasi ya Ubunge katika Jimbo la
Mbagala jijini Dar es Salaam Buluba Mabelele akijaza akiandika jina lake kabla
ya kukabidhiwa fomu ya kuwania ubunge jimbo la Mbagala jijini Dar es Salaam
baada ya kwenda kuchukua fomu hiyo katika ofisi za CCM wilaya ya Temeke.
Kada wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Nicholous
Mpangala ambaye anawania jimbo la Temeke jijini Dar es Salaam akiipitia fomu
hiyo ya kuwania nafasi hiyo baada ya kuichukua leo katika ofisi za Chama hicho
wilayani Temeke.
Mtia nia wa nafasi ya Udiwani kata ya Kijichi
Sabrina Rupia (kulia) akiwa ameshika fomu ya kuwania nafasi hiyo baada ya
kwenda kuichukua leo katika Ofisi za Chama Cha Mapinduzi(CCM) Wilaya ya Temeke.
Mtia nia katika jimbo la Temeke jijini Dar es
Salaam Simon Ruago ambaye amewahi kuwa Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga akipata
maelekezo kutoka kwa Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha
Mapinduzi(UVCCM) Andrew Gwaje(kulia).
Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga
Simon Ruago akijaza moja ya nyaraka baada ya kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya
ubunge jimbo la Temeke jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama Cha
Mapinduzi(CCM) Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam Ally Kamtande akizungumza
na waandishi wa habari kuhusu mchakato wa uchukuaji na urejeshaji fomu ambao
umeanza leo ambapo ametumia nafasi hiyo kuwasisitiza watia nia wote kuzingatia
sheria, kanuni na tararibu zilizowekwa na Chama hicho.
Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama Cha
Mapinduzi(CCM) Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam Ally Kamtande akizungumza
na waandishi wa habari kuhusu mchakato wa uchukuaji na urejeshaji fomu ambao
umeanza leo ambapo ametumia nafasi hiyo kuwasisitiza watia nia wote kuzingatia
sheria, kanuni na tararibu zilizowekwa na Chama hicho.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...