Katibu wa Chama Cha Mapinduzi- CCM Moshi Vijijini, Bi. Miriam Kaaya, akimkabidhi fomu za kugombea ubunge, kada wa chama hicho, Elias Nawera mapema leo 14 Julai.
 Wakili na Mwanasheria nguli ambaye pia ni kada wa Chama Cha Mapinduzi- CCM, Elias Nawera akijaza fomu hiyo mara baada ya kukabidhiwa leo kugombea ubunge jimbo la Vunjo mapema leo 14 Julai.

WAKILI na Mwanasheria nguli ambaye pia ni Kada wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Elias Nawera, leo 14 Julai amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya Chama chake kwa ajili ya kugombea nafasi Ubunge wa Jimbo la Vunjo, mkoani Kilimanjaro.

Nawera amekuwa kwenye siasa na utumishi wa umma kwa muda mrefu ambapo pia amewahi kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Songwe.

Nawera ambaye Mwaka 2005 alikuwa Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa na kwa sasa ni Mjumbe wa Halmashauri  ya Kata ya Kirua Magharibi  na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Moshi Vijijini.

Amekuwa pia akikitumikia  Chama na Jumuia zake  katika majukumu mbali mbali ikiwamo kusimamia Kesi za Chama na hasa Kesi za Uchaguzi baada ya Uchaguzi  Mkuu wa 2010 na 2015. 

Alijiunga na CCM Mwaka 1983 Katika Tawi la Mwenge  Dar es salaam kupitia Umoja wa Vijana wa CCM kama Chipukizi na Mwaka 1987 alikuwa Mwenyekiti wa Chipukizi wa Wilaya ya Chuo Kikuu na  amehudumu katika nafasi mbali mbali  hadi hii leo.

Nawera ni msomi wa taaluma ya sheria ambaye amebobea kwenye masuala ya ushawishi (lobbying), uandishi wa  Mikataba mbali mbali, Majadiliano ya kisheria kwenye masuala ya biashara, Sheria za Udhibiti na Utekelezaji wa huduma mbali mbali za kijamii (utilities).

Pia huduma za kisheria kwa mashirika binafsi (corporates), Wakili wa Masuala ya Kisiasa pamoja na huduma nyingine za kisheria.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...