Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

BAADA ya kuacha chuo miaka 10 iliyopita Clayton Ward (30) amehitimu shahada yake ya kwanza katika Chuo cha MassBay Community nchini Marekani huku akitegemea kuwa mwalimu wa historia katika shule za Sekondari.

 Clayton ni dereva wa magari ya wanafunzi, ambaye familia yake wakiwemo wazazi wake wamefanya kazi hiyo kisha na yeye akajikuta amekuwa dereva wa wanafunzi ambao amekuwa akiwashirikisha namna anavyopenda somo la historia kila alipokuwa akiwaendesha.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la CNN imeelezwa kuwa Clayton akiwa anawaendesha wanafunzi katika mji wa Framingham, Massachusetts wengi wao walikuwa wakimweleza waliyokuwa wakijifunza na alipokuwa na wanafunzi wa sekondari waligundua kuwa Clayton ni mwanahistoria mzuri sana na wakawa wanamuuliza maswali yahusuyo historia.

"Baadhi ya watoto walitamani niwe Mwalimu wao na hiyo ni kutokana na mitazamo tofauti na sauti tofauti na za walimu wao waliowazoea na maongezi yao yanivuta na kunipa nguvu ya kurudi chuo na kutimiza ndoto yangu ya kuwa mwalimu wa historia wa shule za Sekondari" Clayton Ameieleza CNN.

Clayton alianza Chuo mwezi Mei 2019, akisoma masomo ya jioni na kwa njia ya mtandao na hiyo ni baada ya kufanya shughuli yake ya udereva kwa nyakati za mchana.

Ndani ya mwaka mmoja alimaliza masomo yake kwa ufaulu wa kiwango cha juu (GPA 4.0 kwa mujibu w Chuo.)

Clayton ameieleza CNN kuwa asingeweza kupata shahada hiyo bila ushawishi wa watoto hao.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...