Na Said Mwishehe,Michuzi TV
BAKARI Kimwanga ambaye ni Mhariri wa Magazeti ya Kampuni ya New Habari2006 Ltd (RAI na Mtanzania)amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuwania Udiwani katika Kata ya Makurumla wilayani Ubungo jijini Dar es Salaam
Wakati huo huo Mhariri kutoka vyombo vya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Angella Akilimali amejitosa katika kuwania Ubunge Jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam ambapo amechukia fomu ya kuomba ridhaa ya kuwania nafasi hiyo leo katika Ofisi za CCM wilaya ya Ilala.
Kwa upande wake Kimwanga baada ya kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa na Chama chake katika nafasi ya udiwani Kata ya Makurumla ameiambia Michuzi Blog na Michuzi TV kwamba leo Julai 15,2020 amechukua fomu ya kuwania nafasi hiyo.
Amekipongeza na kukishukuru Chama chake kwa kuweka mfumo wa wazi wa uchukuaji fomu na urejeshaji fomu na kwa sasa hawezi kuzungumza mengi zaidi ya kutoa shukrani kwa Chama kwa utaratibu mzuri ambao wameuweka.
"Kwa leo sina cha kusema zaidi ya kueleza tu nimechukua fomu ya kuomba ridhaa ndani ya Chama changu cha CCM kuomba kugombea udiwani Kata ya Makurumla"amesema Kimwanga
Wakati Angel Akilimali akiwa katika Ofisi za CCM Wilaya ya Ilala baada ya kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ndani ya Chama hicho kugombea ubunge Jimbo la Ukonga amesema amefikia uamuzi huo baada ya kujipima na kuona anatosha.
Amesema kwa mujibu wa Chama Chao kimetoa ratiba ya uchukuaji na urejeshaji fomu ,hivyo huu si wakati wa kuzungumza chochote bali wakati utakapofika na kupata ridhaa kutoka kwenye Chama chake atakuwa na chakueleza.
"Chama kimetoa ratiba ya uchukuaji na urejeshaji fomu kwamba mwisho Julai 17 mwaka, hivyo nakwenda kuijaza na kisha na nitairejesha kwa wakati ili kuacha Kura ya maoni itaamua na nani atapeperusha bendera ya Chama ."amesema Angel.
Mhariri wa magazeti ya New Habari 2006 Ltd Bakari Kimwanga akikabidhiwa fomu ya kuomba ridhaa ya kuwania Udiwani Kata ya Makurumla wilayani Ubungo jijini Dar es Salaam na Katibu CCM Kata ya Makurumla Salama Mlaponi(kulia).Kimwanga amechukua fomu hiyo leo Julai 15,2020
Katibu wa CCM Kata ya Makurumla wilayani Ubungo jijini Dar es Salaam( kulia) akijaza risiti ya malipo ya fomu ya udiwani ambayo yamelipwa na Kada wa Chama hicho Bakari Kimwanga
Kada wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Bakari Kimwanga akiwa ameshika fomu ya kuomba ridhaa ya kuwania nafasi ya Udiwani Kata ya Makurumla
Kada wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Angel Akilimali akiwa ameshika fomu ya kuomba ridhaa ndani ya Chama chake kuwania Ubunge Jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam
Angell Akilimali( wa pili kulia) akiwa na baadhi ya wanachama wa CCM ambao wamefika Ofisi za Chama hicho wilaya ya Ilala baada ya kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuwania Ubunge jimbo la Ukonga
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...