Msimamizi wa Miradi wa shirika linalosimamia haki za watoto (Bright jamii initiative), Godwin Mongi akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati akifafanua mambo mbalimbali ya ukatili wa kijinsia kwa binadamu hasa watoto na wanawake. 

Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii
TAFSIRI mbaya za Mila, desturi na mafundisho ya dini yatawa kuwa chanzo cha unyanyasaji, ukiukwaji wa haki za binadamu pamoja na ukatili wa kijinsia.

Hayo yamesemwa na Msimamizi wa Miradi wa shirika lisilo la kiserikali linalosimamia haki za watoto (Bright jamii initiative), Godwin Mongi, akizungumza na michuzi blog jijini Dar es Salaam leo,  amesema kuwa ukatili unaotokea katika jamii ni matokeo na si chanzo au mizizi ya ukatili huo.

Mongi amesema kuwa licha ya kuwepo na matukio mengi ya unyanyasaji pamoja na ukatili katika jamii zetu lakini kumekuwepo na usiri mkubwa kati ya mtendewa wa ukatili huo.

"Lazima kila mmoja aonapo unyanyasaji wa kijinsia na ukatili popote alipo lazima atoe taarifa kwa vyombo vya kutetea na kutokomeza ukatili katika jamii."

"Unatendewa, anatendewa mtu lazima kutoa taarifa hiyo ili kila mmoja aishi salama mahali halipo......"Amesema Mongi.

Hata hivyo mongi amesema kuwa sheria za kutetea haki za wanawake na watoto katika jamii zipo wazi lakini zinashindwa kufanikiwa kwa ufasaha ni kutokana na kutokutoa taarifa kwenye vyombo husika.

"Sheria zipo wazi kabisa zinakataza na adhabu zake zipo wazi kinachofanya sheria ishindwe kuchukua mkondo wake ni mila na destuli pamoja na mafundisho mbalimbali yanayopotosha jamii  na kusababisha ukandamizaji kwa wanawake ambao ndio waathirika wenyewe. "

Licha ya hivyo amesema kuwa licha ya mwanamke kupata ujasiri wakwenda kuripoti katika kituo cha polisi bado anakuwa na fikra za kuwa ndugu zake watamwonaje na jamii itamchukuliaje.

Mongi ametoa mfano wa Zena Mohammed (Shilole) ambaye amevuka hatua na kufunguka kuhusiana na kitendo alichofanyiwa.

"Kitu alichokifanya Shilole ni matokeo tuu licha ya kuwa hatua aliyoipiga kufunguka (kusema) hii ni hatua kubwa aliyoifanya bila kuogopa na kutokufikili jamii itamchukuliaje!."

Wanaofanyiwa ukatili wakichukua hatua kama hii basi ukatili utapungua katika jamii zetu zote. Wanawake waache kukaa kimya kwa vitendo vya kikatili vinavyowatokea." Amesema Mongi.

Licha ya wanawake na watoto kuwa ni watu walio katika kundi maalumu lakini ndio wahanga zaidi katika ukatili wa kijinsia, pia kwa kiasi kikubwa ndio wanaopata unyanyasaji wa kinsia.

Hivyo wanawake kwa pamoja lazima kila mmoja achukue hatua ya kusema na kuvumua unyanyasaji unapotokea katika familia na jamii kwa ujumla.


Shirika lisilo la kiserikali la Bright jamii initiavive ikishirikiana na Men Engage Tanzania mtandao ambao pia Bright Jamii Initiative kwa ufadhili wa Oak Foundation kupitia Sonke Gender Justice wamejikita zaidi katika kusaidia jamii katika kupambana na ukatili wa kijinsia hasa kwa mwanamke na watoto, hata hivyo Mongi amesema kuwa wamewafikia watu wengi na kushirikina na serikali kutoa taarifa kwa vyombo vinavyohusika ili waweze kupata taarifa stahiki.

Licha ya hilo Mongi amesema kuwa wameweza kuzungumza na wanaume ili kushughulikia masuala mazima ya unyanyasaji wa kijinsia ili kumjengea ujasiri mwanamke kutoa taarifa, kutambua haki zake pia kuwajengea uwezo wa kusema hapana kwa unyanyasaji wa kijinsia.

Hata hivyo amesema kuwa wameweza kufanya kazi na wanaume ili waweze kujua kuwa wanachokifanya kuwa sio sahihi na mazungumzo hayo yamefanyika katika ngazi ya jamii kwaajili ya kuwaelewesha jamii kwa ujumla masuala ya kijinsia na ukatili.

"Ukizungumza na jamii ndipo utagundua vyanzo unyanyasaji na ukatili." Amesema Mongi.

Bright Jamii Initiative wameweza kushirikiana na taasisi za kidini ili kusaidia jamii kujiepukana na unyanyasaji na ukatili katika familia, jumuiya unayosali pamoja na jamii kwa ujumla.

"Na kupitia taasisi mbalimbali  zinazomwezesha mwanamke kiuchumi na kupigania haki zao mwanamke anaweza kujitokeza na kusonga mbele pia wanawake wameweza kupata ahueni na kupata msaada ili waweze kusimama wenyewe katika jamii zao na kuondoa mila na desturi kandamizi kwa mwanamke."

Wito kwa jamii kila mtu aishi kwa busara, utashi, na uungwana wa hali ya juu na kuacha kusingizia mila na destuli zetu na tafsiri mbaya za mafundisho ya dini ili kila mtu aone dunia ni mahala pazuri pa kuishi.

Hata hivyo Mongi amesema kuwa kiwango cha busara kinatofautiana kwa kila mtu licha ya kuwa na watu ambao wanatumia vizuri busara zao na wasio tumia vizuri busara zao.

Hulka mbaya ndizo zinasababisha unyanyasaji wa jinsia  katika jamii na kuhisi mwanamke sio kitu na yupo chini yake.

 “Uwanaume ni busara, nguvu hata chizi anazo.” Mongi amemalizia hilo ili kila mtu aishi akitunza haki za watoto pamoja na mwanamke na kutokomeza ukatili na unyanyasaji katika jamii yetu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...