WANAWAKE katika Maeneo mbalimbali hapa nchini wametakiwa kuwa mstari wa mbele kujitokeza kugombea katika nafasi za uongozi katika vyama vya wafanyakazi ili wapate wigo mpana katika ngazi za maamuzi ikiwa ni pamoja na kuleta matokeo chanya kwa wanawake wengine.
Wito huo umetolewa leo jijini Dodoma na msajili wa vyama vya wafanyakazi Bi.Pendo Berege wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku mbili wa wafanyakazi wanawake wa chama cha ( TALGWU) ambapo amesema wanawake hawana budi wainuane na kushirikiana ili kutimiza malengo ya kumfanya mwanamke aweze kuonekana na kuthaminiwa na watu wa kada kada mblimbali za uongozi.
“Bado tunahitaji wanawake wengi kwenye ngazi za uongozi kwenye vyama vya wafanyakazi ,hili nalo tulione kama kipaumbele sisi kama kamati ,hatuwezi kuwa na nyama vya wafanyakazoi 34 ,halafu tuna katibu mkuu mmoja tu mwanamke Sasa tuchukue hatua na tuone ni namna gani tunaweza kuleta mabadiliko.”Amesema
Amesema wanawake hawana budi kushirikiana wenyewe kwa wenyewe na kuinuana pamoja na kuhakikisha wanapeleka ujuzi na elimu watakayoipata katika mafunzo hayo kwa wanawake wengine katika mikoa wanayotoka ili wengi Zaidi waweze kunufaika na kutimiza lile lengo la kumfanya mwanamke aweze kutambua haki zake na wajibu katika eneo lake la kazi.
“Hii fursa tuitumie vizuri tuelewe vizuri yale yote ambayo yataelezwa leo na kuelemishwa na tutakaporudi kwenye mikoa yetu ,ninaomba haya tutakayojadili muyapeke kwa wenzetu ambao hawakuweza kufika ,tusikae nayo kwenye pochi zetu.”Amesisitiza
Awali akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo mwenyekiti wa kamati ya ushauri wafanyakazi wanawake TALGWU Taifa Bi. Beatrice Njawa amesema kuwa wanawake bado wamekuwa wanakabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo rushwa ya ngono,mfumo kandamizi ,na mila potofu hali ambayo huleta usumbufu na hivyo kuwadhalilisha kijinsia na kudhoofisha hali ya utoaji wa huduma katika maeneo yao.
“Tunaomba serikali kukemea vitendo hivi na kuwaelekeza viongozi kuzingatia sheria,miongozo na taratibu za kazi ili kulinda utu na thamani ya mwanamke katika eneo hilo.”Amesema .
Hata hivyo amesisitiza kuwa pamoja na juhudi mbalimbali zinazofanywa na serikali katika kumuinua mwanamke ,lakini bado kumekuwa na uwakilishi mdogo wa wanawake katika ngazi za maamuzi ,hivyo kusababisha uwepo wa mfumo dume hali inayowaletea hofu na uwoga wafanyakazi wanawake kushika nafasi mbalimbali za uongozi zitakazowapa fursa ya kushiriki katika ngazi za maamuzi.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...