Jaji Kiongozi
wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi akiongoza kikao
cha Baraza la Elimu ya Sheria la Tanzania Bara, kwa njia ya Mkutano
Mtandao leo Jijini Dar es Salaam huku baadhi ya wajumbe wawili
wakishiriki kwa mtandao nje ya jiji hilo. Jaji Kiongozi ambaye ni
Mwenyekiti wa baraza hilo, ameongoza kikao hicho cha tathmini ya
mchakato wa kupokea maombi , usahili wa kuwapokea na kuwakubali mawakili
wapya uliofanyika hivi karibuni.
Mjumbe wa
kikao hicho, Dkt. Erasmo Nyika ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam Shule ya Sheria kwa Vitendo (Law School )akichangia hoja.

Katibu wa
Baraza la Elimu ya Sheria la Tanzania Bara, ambaye pia Naibu
Msajili Mkuu Mwandamizi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Kuu, Mhe.
Messe Chaba, akitoa tathmini ya mchakato huo.
Mjumbe wa kikao hicho, Aisha Sinda ambaye ni Wakili wa Kujitegemea akizungumza jambo kwenye kiako hicho.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...