Na Munir Shemweta, WANMM DODOMA

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amepokea msaada wa Kompyuta 10 zenye thamani ya milioni 12 kutoka Benki ya Azania.

Msaada huo ulipokelewa leo tarehe 10 Julai 2020 katika ofisi za ardhi mkoa wa Dodoma na kushuhudiwa na viongozi mbalimbali wa Wizara akiwemo Katibu Mkuu Mary Makondo.

Akizungumza baada ya kupokea msaada huo, Waziri Lukuvi aliishukuru Benki ya Azania kwa msaada huo alioueleza kuwa utasaidia sana kwenye huduma za sekta ya ardhi hasa katika ofisi za ardhi za mikoa zilizoanzishwa hivi karibuni.

Alisema, benki ya Azania imekuwa ikiunga mkono jitihada za Wizara kusaidia vifaa na kuzitaka taasisi nyingine kuiga mfano wa Benki ya Azania katika kusaidia juhudi za serikali kusogeza huduma za ardhi karibu na wananchi.

Kwa mujibu wa Lukuvi, hivi sasa wizara yake baada ya kuanzisha ofisi za ardhi katika mikoa inafanya jitihada mbalimbali kuhakikisha ofisi hizo zinakuwa na vifaa vya kutosha kwa lengo la kuwawezesha watendaji wa ofisi hizo kufanya kazi kwa ufanisi.

Kwa upande wake Meneja wa Benki ya Azania mkoa wa Dodoma Makalla Mbura alimueleza Waziri wa Ardhi kuwa msaada uliotolewa moja ya juhudi za benki hiyo kusaidia jitihada mbalimbali zinaziofanywa na wizara ya ardhi kwenye sekta ya ardhi.

Makalla aliongeza kwa kusema kuwa, benki hiyo itaendelea kuunga mkono jitihada za wizara katika masuala mbalimbali ya huduma za sekta ya ardhi kwa kutoa msaada pale unapohitajika.
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akipokea msaada wa Kompyuta 10 zenye thamani ya shilingi milioni 12 kutoka kwa Meneja wa Benki ya Azania mkoa wa Dodoma Makalla Mbura  leo tarehe 10 Julai 2010. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Mary Makondo.
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza baada ya kupokea msaada wa Kompyuta kumi zenye thamani ya milioni 12 kutoka kwa Meneja wa Benki ya Azania mkoa wa Dodoma Makalla Mbura (Kulia) leo tarehe 10 Julai 2010. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Mary Makondo.
 Meneja wa Benki ya Azania mkoa wa Dodoma Makalla Mbura akizungumza baada ya kutoa msaada wa Kompyuta 10 zenye thamani ya shilingi milioni 12 kwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi leo tarehe 10 Julai 2020. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Mary Makondo.
 Baadhi ya watendaji wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakifuatilia makabidhiano ya msaada wa Kompyuta kumi zenye thamani ya shilingi milioni 12 kutoka Benki ya Azania leo tarehe 10 Julai 2020 jijini Dodoma.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi pamoja na Katibu Mkuu wake Mary Makondo wakisoma kijarida kinachoelezea masuala ya usajili wa hati alipotembelea ofisi ya Msajili wa Hati leo tarehe 10 Julai 2020 jijini Dodoma. (PICHA ZOTE NA MUNIR SHEMWETA WIZARA YA ARDHI)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...