Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe (kwanza kushoto) akimsikiliza Meneja wa Vipimo Mkoa wa Pwani, Alban Kihulla mara baada ya kutembelea kituo cha Wakala wa Vipimo Misugusugu Mkoa wa Pwani kujionea shughuli mbalimbali wanazofanya. Pichani ni mashine ya kupima dira za maji zinazotumiwa taasisi zinazotoa huduma za maji. 
Picha zote na Cathbert Kajuna- Kajunason/Michuzi Tv
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe (kwanza kulia) akimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu-WMA, Dkt. Ludovick Manege (katikati) mara baada ya kutembelea kituo cha Wakala wa Vipimo Misugusugu Mkoa wa Pwani kujionea shughuli mbalimbali wanazofanya.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe (wa pili toka kushoto) akiangalia jinsi shughuli za upimaji wa matanki ya mafuta unavyofanyika.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe (kwanza kushoto) akimsikiliza Meneja wa Vipimo Mkoa wa Pwani, Alban Kihulla mara baada ya kutembelea kituo cha Wakala wa Vipimo Misugusugu Mkoa wa Pwani kujionea shughuli mbalimbali wanazofanywa. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe  akizungushwa sehemu mbai mbalimbali za jengo na Afisa Mtendaji Mkuu-WMA, Dkt.Ludovick Manege.
Afisa Mtendaji Mkuu-WMA, Dkt.Ludovick Manege akifafanua jambo kwa wanahabari  Wakala wa Vipimo Misugusugu Mkoa wa Pwani. 
Katibu Mkuu wa Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe akizungumza na wanahabari mara baada ya kumaliza ziara yake katika kituo cha Wakala wa Vipimo Misugusugu Mkoa wa Pwani. 

 Na Cathbert Kajuna - Kajunason/Michuzi Tv.
WAKALA wa Vipimo Tanzania (WMA) wamejipanga ifikapo mwezi wa kumi watakuwa wameshamaliza ujenzi wa jengo la kuhifadhi mtambo wa kupima mita za umeme.

Kwasasa wamekuwa wakipima magari ya mafuta na dira za maji lakini kwa kufikia mwezi wa kumi watakuwa wameshaanza kupima dira za umeme kwasababu tayari taratibu za manunuzi zimekamilika.

Kauli hiyo imetolewa na Afisa Mtendaji Mkuu -WMA, Dkt. Ludovick Manege wakati akitoa maelezo machache kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe mara baada ya kutembelea kituo hicho kilichopo Misugusugu Mkoa wa Pwani. 

Dkt. Manege amesema kuwa utaratibu wa kuwepo kwa mtambo wa kupima mita za umeme ulikwishaanza na kufikia mwishoni mwa mwaka huu utakuwa tayari umeshakamilika. 

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe mara baada ya kutembelea kituo hicho amewataka WMA washirikiane na Tanesco pamoja na TPDC ili kuweza kufanikisha jambo la kupima mita zinazoweza kutumika katika matumizi. 

 “WMA wameanza mkakati wa kupima mita za umeme, niombe suala hili lifanyiwe kazi kwa haraka lile jengo ambalo linatakiwa lijengwe kwa ajili ya kuhifadhi mtambo wa kupima mita za umeme lijenge na ikiwezekani kabla ya mwisho wa mwaka huu”. Amesema Prof. Shemdoe. 

 Aidha Prof. Shemdoe ameomba kuanza mchakato wa kupata mtambo mwingine ambao utasaidia kupima mita za gesi zinazotumika viwandani na pengine ambazo tumeanza kuzitumia majumbani ili waweze kulipa kutokana na matumizi sahihi. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...