Na Khadija Seif, Michuzi TV

KATIKA Wanamuziki wanaoliunda kundi la wasafi (WCB) huwezi kuacha kumtaja nyoya anayekuja juu kwa kasi Zuhura Omary Kopa a.k.a Zuchu (pichani akiwa na mama yake Khadija Kopa) kwa sauti yake ya mikogo na nakshinakshi zote za kuvutia.

Zuchu ni Msanii ambae tayari kwa Sasa ametoa album (EP) ambayo imepokelewa vizuri na mashabiki ikiwa ina nyimbo takribani 7, ikiwemo Ashua aliyomshirikisha Msanii mbosokhan, hakuna kulala, nisamehe, kwaru, Wana, Raha, pamoja na Mauzauza aliyomshirikisha mama yake mzazi,Khadija kopa.

Aidha  julai 18 zuchu amejipanga kuwapa burudani na kukata kiu mashabiki wake.

"Kwa sababu ndio itakua shoo yangu ya kwanza tangu nilipoingia rasmi kwenye muziki huu, basi wategemea vitu vizuri kutoka kwangu."

Hata hivyo Zuchu amewashukuru mashabiki zake kwa kumpokea vizuri kwenye Ep yake ya Iam Zuchu, na imemfanya apate madili mengi kwa Sasa ndani na nje ya nchi.

"Bila mashabiki mimi si kitu, nimepokelewa kwa mapenzi makubwa Sana ,wamenipa nguvu kubwa ya kuendelea kufanya vizuri katika tasnia ya muziki."

 Zuchu amesema anafarijika kuona Rais John Magufuli anaelewa na  anapenda kazi zake na kutokana na hilo imekua mara ya kwanza kutumbuiza wimbo mbele ya Rais.

"Naweza kusema Rais Magufuli ni shabiki mkubwa wa kazi zangu, ndio maana sikuona zawadi ya kumpa zaidi ya kumtungia wimbo ambao kwa Sasa unasikika Sana kwenye shughuli za chama."

Pia Zuchu amewaomba mashabiki zake waje kwa wingi katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam kwa ajili ya shoo yake ya shukrani kwa mashabiki zake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...