Wadau mbalimbali wa kilimo cha zao la korosho nchini  wameonesha kuvutiwa  na huduma mpya ya NBC Shambani huku wakibainisha ujio wa huduma hiyo maalumu kwa ajili ya wakulima utaondoa changamoto za muda mrefu  ikiwemo kutopata mikopo kwa wakati  sahihi.
Wakizungumza wakati walipotembelea banda la huduma za benki hiyo kwenye mkutano mkuu wa wadau wa korosho uliofanyika mwishoni mwa wiki mkoani Lindi, baadhi ya wadau wa zao hilo wakiwemo wakulima, wafanyabiashara wa pembejeo za kilimo na wasafarishaji wa zao hilo walisema miongoni mwa changamoto zinazowakabili kwa sasa ni kutopata mikopo kwa wakati sahihi hivyo wanaamini ujio wa huduma hiyo mpya utaondoa changamoto hiyo.
“Licha ya uwepo wa huduma nyingi za kibenki kwa ajili ya wakulima bado tumeendelea kukabiliwa na changamoto kadhaa za huduma za kifedha ikiwemo ucheleweshwaji wa mikopo na tunapoipata inakuwa sio wakati sahihi na hivyo kusababisha wengi wetu kuitumia kwa matumizi yasiyokusudiwa. Ni matarajio yetu ujio wa huduma NBC Shambani utatatua changamoto hii na sisi tupo tayari kuiopokea,’’ alisema Bw Salum Muhila, mkulima wa korosho kutoka wilaya ya Liwale, mkoani Lindi.
Awali, akifafanua kuhusu huduma hiyo kwa wadau hao, Mkuu wa Kitengo cha wateja Wadogo na  wa Kati kutoka Benki ya NBC  Bw Raymond Urassa alisema inalenga wadau wote wanaojihusisha na mnyororo wa biashara ya Kilimo wakiwemo wasambazaji wa pembejeo za kilimo, wakulima na wasafirishaji wa mazao ya kilimo na tayari imepoanza kutumiwa kwa wingi na wakulima wa zao lq ufuta.
“Kwa kuwa NBC Shambani imekuja mahususi kwa ajili ya wadau wa kilimo tafsiri yake ni kwamba ufanisi wake upo kwenye kutatua changamoto hasa zinazowagusa wadau hao ikiwemo kupata mikopo kwa wakati sahihi ili mkulima autumie mkopo huo kufanya kile hasa kinachotakiwa kufanywa kwa wakati huo,’’ alisisitiza
Alibainisha huduma hiyo inatoa fursa kwa wadau hao kuwa na akaunti ya  vikundi vya wakulima kama vile AMCOS na vikundi vingine pamoja na akaunti ya mkulima mmoja mmoja.
 “Akaunti  ya NBC Shambani kwa vikundi vya wakulima inawawezesha kuweka fedha bila ada  ya uendeshaji wa akaunti huku pia vikundi vikifaidika kwa  faida nyingi ikiwemo kutokatwa gharama za uendeshaji wa akaunti kila mwezi, kupata taarifa za akaunti bure sambamba na kutokatwa makato ya kuhamisha fedha wakati wa kulipa wakulima  wenye akaunti NBC,’’ alifafanua.
Akizungumza kwenye mkutano huo, Waziri wa Kilimo Bw Japhet Hasunga alibainisha kuwa katika kubabiliana na changamoto kadhaa zinazowakabili wakulima ikiwemo kutotambulika rasmi kwenye taasisi za kifedha tayari serikali imeanza kutoa vitambulisho maalum kwa ajili yao vitakavyowatambulisha hususani wanapohitaji huduma za kifedha.
“Vitambulisho hivyo vya kisasa vitakuwa na ‘chip’ maalumu itakayobeba taarifa zote muhimu kuhusu mkulima hatua ambayo tunaamini itazirahisishia taasisi za fedha mlolongo mrefu wa kukusanya taarifa za wadau hao na hivyo kuwapatia mikopo kwa wakati,’’ alisema Waziri Hasunga ambae katika mkutano huo alikabidhi vitambulisho hivyo vya mfano kwa wakulima 15 wa awali.
“Zaidi pia kwasasa serikali tunatathimini upya sera ya masoko ikiwemo suala zima la kilimo cha mkataba ili wakulima wetu waweze kujua bei za bidhaa zao mapema kabisa,’’ alibainisha.
 Mkuu wa Kitengo cha wateja Wadogo na  wa Kati kutoka Benki ya NBC  Bw Raymond Urassa akielezea kuhusu huduma mbali mbali za kilimo zinazotolewa na benki hiyo ikiwemo huduma mpya ya ‘NBC Shambani’ mbele ya wadau wa zao korosho nchini wakati wa mkutano mkuu wa wadau hao  uliofanyika  mkoani Lindi hivi karibuni. Benki hiyo ilikuwa moja ya wadhamini wakuu wa mkutano huo ambao pia ulihudhuriwa na Waziri wa Kilimo Bw Japhet Hasunga.
 Meneja wa Benki ya NBC Tawi la mkoa wa Lindi Bw Iovin Mapunda (Kulia) akizungumza na Bw Salum Muhila, mkulima wa korosho kutoka wilaya ya Liwale, mkoani Lindi kuhusu huduma za benki hiyo kwa wadau wa kilimo cha korosho ikiwemo huduma mpya ya benki hiyo ya NBC Shambani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...