Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii
SHIRIKISHO la vyombo vya Moto nchini (AAT) likishirikiana na shirikisho la vyombo vya moto duniani (FIA) pamoja na shirika la Kimataifa la Michelin wameandaa mafunzo ya siku moja kwa madereva wa kujihami (Difensive Driving) kwa madereva zaidi ya 600 wa jijini Dar es Salaam.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Rais wa Shirikisho la vyombo vya Moto nchini (AAT), Nizar Jivan amesema madereva hao ni pamoja na madereva wa Malori, Mabasi ya Abiria, Mabasi ya Wanafunzi na Madereva wa Magari ya Wagonjwa (Ambulance).

Amesema kuwa mafunzo hayo yataendeshwa na wataalamu walio chini ya Shirikisho la vyombo vya Moto nchini (AAT), Mako makuu ya Usalama Barabarani nchini, Kituo cha Zimamoto na Uokoaji na ofisi ya Huduma ya kwanza Tanzania.

Licha ya hilo amesema kuwa mafunzo hayo hayatakuwa na gharama yeyote kwa watakaohudhuria ikiwa ni majukumu ya Shirikisho la vyombo vya Moto nchini (AAT) na shirikisho la vyombo vya moto duniani (FIA).

Jivan amesema lengo la mafunzo hayo ni kupunguza ajari za barabarani, kuelewa alama mpya za barabarani pia amesisitiza mafunzo hayo ni mhimu na yatadumu kwa miezi mitatu yakishirikisha madereva kutoka kampuni 30.

Jivan amesema watakaotoa mafunzo hayo ni Trafiki Mkao Makuu, SP Deus Sokoni, Trafiki Mkao Makuu, SP Abel Swai, Mkufunzi Mwandamizi Kutoka ofisi ya AAT, Samwel Salahe, Mathew Nkanyemaka kutoka Paramedic, Christine Charles na Fares Kauli kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

Pia kutakuwa na wawakilishi kutoka Ofisi ya Utamaduni na Michezo wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mwakilishi kutoka Michelin Tanzania, Wawakilishi mbalimbali kutoka katika makapuni, Vyomo vya habari pamoja na Wakufunzi wa Mafunzo.
 Rais wa shirikisho la vyombo vya Moto nchini (AAT), Nizar Jivani akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati akitambulisha mafunzo kwa madereva wa vyombo vya moto yatakayofanyika hivi karibuni kwa m,adereva wa jiji la Dar es Salaam.
Meneja Mradi - Uendeshaji wa kujihami, Yusuf Ghor -  akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

Mrakibu wa Polisi, Deus Sokoni akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo huku wakishirikiana kwa ukaribu katika kutoa mafunzo kwa madereva wa jijini la Dar es Salaam hivi karibuni.

Rais wa AAT, Nizar Jivani akimkabidhi kofia Ngumu Mrakibu wa Polisi , SP Deus Sokoni leo.
Wakiwa katika Picha ya pamoja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...