Mtaalamu wa Huduma Ndogo za Fedha kutoka Wizara ya Fedha na Mipango,
Bi. Janeth Hiza (kushoto), akitoa elimu ya Sheria ya huduma hiyo kwa
wanawake kutoka Bariadi Mkoani Simiyu walio katika vikundi mbalimbali
vya VICOBA, walipotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika
Maonesho ya Nanenane Kitaifa, viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.
Wakazi wa Mkoa wa Simiyu Bi. Mwinza Maghembe na Mbula Mayenga, wakipewa
elimu ya huduma ndogo za fedha kutoka kwa Mtaalamu wa Sekta hiyo wa
Wizara ya Fedha na Mipango. Bi. Limi Burugu (kushoto), walipotembelea
Banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa,
viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.
Wakazi wa Bariadi Mkoa wa Simiyu (kushoto) wakipewa maelezo juu ya
mifumo ya malipo ya Serikali kutoka kwa mtaalamu wa mifumo hiyo wa
Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Chilumba, walipotembelea Banda
la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa,
viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.






(Picha na Peter Haule, WFM)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...