Na Said Mwishehe, Michuzi TV

WASANII zaidi ya 109 pamoja na bendi karibu zote nchini Agosti 15 mwaka huu wa 2020, watakuwa Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam ambako litafanyika tamasha kubwa ambalo limeandaliwa na Chama Cha Mapinduzi(CCM) kwa ajili ya kuzindua nyimbo za kampeni.

Kwa mujibu Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole amesema leo Agosti 5,2020 jijini Dar es Salaam kwamba nyimbo hizo zitakuwa ni kabla ya kampeni, wakati wa kampeni na baada ya kampeni.

"Agosti 15 mwezi huu tutakuwa na jambo letu pale Uwanja wa Uhuru, tutakuwa na tamasha kubwa sana la ndani kutambulisha nyimbo za CCM, nyimbo kabla ya kampeni, wakati wa kampeni na baada ya kampeni, Wasanii 109 ambao wote ni wa nchi hii, bendi zetu watakuwa pale.Kuna jambo pale Uhuru tutalifanya.

"Kwa hiyo Watanzania wote wanaoamini acha kazi iendelee basi tukutane Agosti 15 mwaka huuu Uwanja Uhuru jijini Dar es Salaa.Orodha ya wasanii watakaokuwepo ni ndefu sana lakini miongoni mwao atakuepo Diamond Platnuz na kundi lake lote, atakuwepo King Kiba na kundi lake, atakuwepo Hamornize na kundi lake.

"Kuna na Ditto na THT, Peter Msechu, Kalapina, Shilole, Nandy, Msaga Sumu, Dudubaya ,Linah Sanga, Country Boy, Chid Benz na wasanii wengine kibao.Hata TID Mnyama atakuwepo siku hiyo, Masanja Mkandamizaji.

"Afande Sele atakuwepo, yaani wasanii karibia wote mnafaowafahamu watakuwepo siku hiyo.Kutakuwa na bendi pia , Ally Choki atakuwepo,"amesema Polepole wakati anazungumzia tamasha hilo ambalo litaanza saa nne asubuhi hadi kesho yake.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...