Na Woinde Shizza, Michuzi Tv Arusha .


 Kaimu Msajili wa bodi ya nyama Tanzania Imani Sichalwe ameiomba serikali kununua ndege ya mizigo kwa ajili ya kusafirisha   nyama nje ya nchi kwani soko la nyama nje ni kubwa sana



Sichalwe ameyasema hayo leo wakati akizungumza na Waandishi wa habari ndani ya Banda lao lililopo katika maonesho ya nane nane yanayofanyika katika viwanja vya Themi njiro jijini Arusha, Ambapo alibainisha kuwa kuwepo kwa ndege ya mizigo kutasaidia kupunguza gharama ya usafirishaji nje ya nchi



Alisema kuwa iwapo itakuwepo ndege ya Taifa kutakuwa na uhakika wa kago ya kusafirishia mizigo pia itamsaidia kuimarisha biashara ya nyama nje ya nchi kwani mizigo ya nyama itakuwa inafika katika nchi husika kwa wakati



Aidha pia alizitaka Halmashauri zote hapa nchini kujenga viwanda pamoja na machinjio Bora ya nyama ili nyama zinazopatikana hapo zisimamiwe vyema ziwe na ubora ambao unaweza kuuzwa Ndani ya nchi nanje ya nchi .



“hapa nchini kwetu tuna mifugo mingi sana ambayo tukiwa na viwanda vyetu pamoja na machinjio tukawa na ndege yetu tukapeleka nje ya nchi tutapata  faida kubwa mno ambayo itasaidia kukuza pato la nchi yetu “alibainisha Sichalwe



Aidha pia aliwataka wananchi kujijengea tabia yakula nyama Mara kwa Mara kwani ulaji nyama kwa wingi unasaidia mambo mengi ikiwemo kutengeneza akili ,unasaidia kutengeneza vichocheo vingi vya mwili ,inakupa vitamini mbalimbali Kama vile zinki,ambapo alibainisha kuwa binadamu waliubwa kula nyama Hivyo wanapaswa kula nyama ya kutosha



Alifafanua kuwa kishe mtu mmoja anatakiwa kula nyama kilo 50 kwa mwaka Ila hadi Sasa hapa nchini Tanzania ,mtu mmoja akila nyama nyingi kwa mwaka Ni kilo 15hivyo Ni vyema kila mtanzania akajitaidi kula nyama nyingi kadri awezavyo ili afikie malengo



Alibainisha kuwa katika kuelekea soko la kimataifa  kila mfugaji anatakiwa kufuga kisasa kwa kuacha kufuga mifugo mingi isiona tija badala yake badala ya kufuga mifugo 2000 ambao akiwauza hapati faida ni boda mfugaji akafuga mifugo kama 10 lakini ambayo ataweza kuihudumia vyema na akiipeleka sokoni itampa faida kubwa zaidi



Wakati huo huo alitumia muda huo kuwaonya wenye mabucha wote ambao bado wanatumia magogo kuuzia nyama na kusema kuwa kwa sasa hivi kuna mashine maalumu ya kukatia nyama  hivyo ni marufuku mwenye bucha yeyote kutumia vigogo kukata nyama na iwapo atakutwa anatuia vigogo kufanya hivyo atalipishwa faini ya shilingi laki moja au kuchukuliwa hatua zingine za kisheria.
Kaimu Msajili wa bodi ya nyama Tanzania Imani Sichalwe akiongea na waandishi wa habari ndani ya banda lao la maonesho lililopo katika viwanja vya Themi Njiro mkoani Arusha ,sehemu ambayo maonesho ya 27 ya nane nane yanafanyika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...