Na Said Mwishehe, Michuzi TV
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Humprey Polepole amesema amesikitishwa na kuhuzunishwa na kitendo cha Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) kuushusha hadhi wimbo wa Taifa kutokana na kuongeza maneno yao.
Polepole ameviambia vyombo vya habari leo Agosti 5,2020, jijini Dar es Salaam kwamba Chama kimoja cha upinzani(CHADEMA) kilikuwa kimefanya mkutano wake. "Sikuwa nataka kusema lakini kimetuuma, ujue nchi hii inatambulishwa kwa jina lake,inaitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
"Unapotembea pasipoti yako inaonesha unatoka Tanzania, kingine kinachotutambulisha kwa watu ni wimbo wa Taifa.Uwe Mmakonde, Mzaramu, Msukuma, uwe Muislamu, uwe Mkristo na hata uwe mshirikina wimbo wa Taifa ndio unatutambulisha Watanzania.
"Kwa mfano sisi Wakristo Sala ya Baba yetu uliyembinguni huwezi kuibadilisha hata kidogo, Hata kama unampenda vipi baba yako wa hapa duniani , huwezi kusema baba yangu uliye duniani.Haiwezekani hata kidogo, CCM tunazo nyimbo nyingi sana , hivyo huu mmoja hatuwezi kuunajinsi, huu wimbo tunamuomba Mungu aibariki Tanzania. Wimbo wa Taifa ukipigwa tunaweka mikono chini, wimbo hu ni sala,"amesema Polepole.
Amesisitiza kuwa hicho chama(CHADEMA) kinamatatizo na anashindwa kukielewa.Hawa jamaa wana matatizo juzi jamaa yao karudi vurugu mtindo mmoja.Hiki Chama nimeshindwa kukielewa.Nidhamu ni zero,kutii sheria ni zero.Sasa wamekuja na kuharibu wimbo wa Taifa, halafu wanakuja na hoja ya kuuliza wapi kuna sheria.Hivi wapi imeandikwa usichukue mke wa kaka yako.Mke wa kaka yako ni shemeji yako hata kama haiko kwenye sheria.
"Jambo linaweza lisiliwe kuwa sio la kisheria lakini lina uhalali, wimbo huu wa Taifa una uhalali.Kabla ya kupata dhamana tayari wameubadilisha wimbo wa taifa na kuwa wimbo wao.Wafahamu sio kila kitu kilipata uhalali wa kisheria.
"Kwa viongozi kinachotakiwa ni kupata uhalali. Ukiwa na ndugu yako wa aina hii ni hasara omba lisitokee.Wimbo wa taifa unaharibiwa halafu wanajimbwafai.Ndugu wanahabari mtufikishie kwa Watanzania hili jambo linatuuma. Wakati wa Corona tuliimba huu wimbo, Chama ambacho hata uhalali hakina,basi tu tunaacha.Kama nilivyosema ukiwa na ndugu hasara unafanyaje,"amesema Polepole.
Kwa kukumbusha tu, kumeibuka mjadala mkubwa nchini, baada ya CHADEMA kamua kuongeza maneno kwenye wimbo wa Taifa, huku Chama hicho kikisema wamefanya hivyo kwasababu hakuna sheria inayokataza kufanya hivyo.

Hata hivyo Polepole ameongeza ni makosa kubeza wimbo wa taifa na kuuteremsha hadhi."Najua hawataomba radhi, niko tayari kubeti,hawataomba radhi.Chama hiki kina matatizo makubwa sana.Tulipojenga miundombinu walibeza, tulipojenga Fly Over wamebeza na juzi jamaa yako amepita katika hiyo hiyo Fly Over.
"Kila kinachofanyika wanasema ni maendeleo ya vitu.Meli ya Mv Victoria imekamilika inakwenda Kagera hdi Mwanza kwa saa sita lakini hawa jamaa wanabeza tu.Bombadiar itaanza kwenda Ruvuma unasema maendeleo ya vitu.Unakuwa na Chama linafanya madudu lakini unaishi nalo maana tuaambiwa tuwe na uvumilivu wa kisiasa,"amesema Polepole na kuongeza kama hiyo haitoshi wameamua kubeza na wimbo wa Taifa.
Amesisitiza kwa hicho ambacho CHADEMA wamekifanya , ni kitendo kinachoumiza na kusikitisha sana lakini anawaachia Watanzania ndio wenye wimbo wao na hakika hawakufurahishwa na kitendo hicho.
Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali wakimsikiliza KATIBU
wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Humprey Polepole
alipokuwa akizungumza leo jijini Dar,ambapo alisema kuwa amesikitishwa na kuhuzunishwa na kitendo cha Chama cha
Demokrasia na Maendeleo(Chadema) kuushusha hadhi wimbo wa Taifa kutokana
na kuongeza maneno yao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...