Tofali pilipili ambalo linatengenezwa kwa mavi ya tembo pamoja na pilipili kwaajili ya kuzuia tembo wasiingie shambani kuharibu mazao likiwa tayari kwa matumizi,lipo katika banda la halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro katika maonyesho kanda ya kaskazini viwanja vya Themi Njiro.
Chrisriani Cyril Rimoi Mtaalamu wa wanyama pori halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro:Mnyama Tembo huwa hapatani na pilipili kabisa sana
Taa inayotumika kufukuzia wanyama wakali ambayo huwasha kimulimuli nyakati za usiku ipo banda la Halmashauri ya (w)Ngorongoro
TEKNOLOJIA YA 'TOFALI PILIPILI' KIBOKO YA TEMBO
Na.vero Ignatus ,Arusha
Idara ya Maliasili halmashauri ya Ngorongoro imewataka wakulima na wafugaji ,kutumia teknolojia ya tofali pilipili ili kudhibiti wanyama kama tembo kuingia katika mashamba yao na kuharibu mazao
Hayo yamesemwa na Chrisriani Cyril Rimoi Mtaalamu wa wanyama pori kwamba wapo kwenye maonyesho ya nanenane kanda ya kaskazini lengo likiwa ni kutoa elimu kwa wananchi namna ambavyo teknolojia hiyo ya tofali pilipili,inavyoweza kukabiliana na wanyama pori wakali, ili kuweza kunusuru mifugo pamoja na mazao, yasiweze kuharibiwa bila kusababisha madhara kwa wanyama
Amesema kwa asili mnyama tembo hapendi pilipili ,hivyo tofali hilo linapochomwa hata akiwa kwenye umbali wa mita mia moja na kuendelea anakuwa tayari ameshahisi harufu, hivyo hataweza kusogelea mahali ambapo tofali hilo lipo, bali atageuza muelekeo na kurudi porini
Amesema wilaya ya ngorongoro ni ya uhifadhi sehemu limezungukwa na hifadhi na kuna wanyama wengi,hivyo baada ya kutumia teknolojia hiyo imeonyesha wazi kwamba imefanyakazi vizuri na imewasaidia sana wananchi wa eneo hilo siyo wakulima pekee hata kwa wafugaji pia.
Mtaalam huyo alisema kuwa tofali hilo linatengenezwa kwakutumia kinyesi cha tembo pamoja na pilipili ,ambapo likichomwa moto linasaidia tembo wasifike karibia na mashamba, ambapo wakulima wakitumia teknolojia hiyo itawasaidia kuinua kipato chao kwa uhakika zaidi
''Mnyama tembo anaweza kuharibu shamba kwa muda mfupi sana,atakapoingia na huwa anaharibu kwelikweli .Alisema mtaalam huyo wawanyamapori''
Amesema hadi sasa teknolojia hiyo waweweza kuitumi kwa wakulima takribani kwa miaka mitano sasa,na inafanya vizuri ndiyo sababu iliyowalazimu kushiriki maonyesho kwaajili ya kutoa elimu kwa wakulima na wafugaji
Namna ya kutumia tofali pilipili inategemea na ukubwa wa shamba umbali kati ya tofali moja hadi jingine ni mita 10,inategemea upande ambao wanyama wanaingilia, kama ni hekta moja eneo la mraba la hatua 70 mkulima anaweza akaweka 7 inategemea wanyama wanaingia kwa hiyo kama ni mzunguko mkulima atazidisha mara nne.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...