KUFUATIA Mlipuko wa bandari katika mji mkuu wa Beirut, nchini Lebanon Shirika la ndege la kimataifa Emirates limendelea kutoa huduma muhimu na misaada kwa wahanga wa mlipuko huo, na hiyo ni pamoja na kutoa ndege  zaidi ya 50 zikiwemo ndege za mizigo ambazo zimekua zikisafirisha huduma muhimu nchini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji Shirika la Emirates Sheikh Saeed Al Maktoum imeeleza kuwa kufuatia janga hilo la dharura kidunia, Lebanon imekua ikihitaji misaada ya dharura na wao kama shirika wakaona ni vyema kutoa misaada ya kibinadamu ikiwemo chakula, malazi na huduma za afya kwa raia wa Lebanon.

Imeelezwa kuwa misaada hiyo ya dharura ambayo imeendelea kiwasilishwa na ndege za mizigo za shirika hilo ni pamoja na vifaa vya afya, vyakula na huduma nyingine za muhimu na za dharura na hiyo ni pamoja na kuweka punguzo la asilimia 20 za usafirishaji wa mizigo ya bandari ya Beirut.

Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa Shirika hilo linawapa nafasi watu wote kote duniani  kutoa msaada wa hali na mali kupitia taasisi ya shirika hilo na kwa miezi mitatu ya kutoa misaada hiyo Emirates kupitia "Emirates Airlines Foundation" itahakikisha misaada yote ya dharura ikiwemo vyakula, vifaa tiba vinawafikia walengwa na hiyo ni kwa kushirikiana na asasi mbalimbali za kiraia za Lebanon ili kuhakikisha mahitaji hayo muhimu yanawafikia walengwa.

Takwimu zinaonesha kuwa shirika la ndege la kimataifa la Emirates kupitia ndege  limekua mstari wa mbele katika kusafirisha  misaada mbalimbali nchini Lebanon ikiwemo vyakula, nguo na vifaa tiba ambavyo vilitolewa na taasisi mbalimbali za umoja wa nchi za kiarabu (UAE.)

Taarifa hiyo pia imeeleza azma yake ya kuendeleza ushirika wake katika jamii kwa namna mbalimbali ambapo hadi sasa zaidi ya miradi 30 ya kibinadamu imekua ikiendeshwa katika nchi 16.

Shirika la ndege la kimataifa la Emirates kwa miaka mingi sasa limekua likishiriki shughuli mbalimbali za kijamii na tangu mwaka 2013 Emirates A 380 imekua ikisafirisha zaidi ya tani 120 za vyakula kwa wahitaji mbalimbali.

Shirika la ndege la kimataifa la Emirates lilianza kutoa huduma nchini Lebanon tangu mwaka 1991, huku safari za Beirut, Dubai zikiwa mara tatu kwa wiki kupitia Boeing 727 na sasa safari hizo zinapatikana mara mbili kwa siku kupitia Boeing 777.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...