Mganga mkuu Manispaa ya Ubungo Peter Nsanya akikabidhiwa Vifaa vya afya na Mwenyekiti wa bodi ya Goba Roads Runners(GRR), Fritz Msanjo ambavyo ni Barakoa, Grovis, na vifaa ya kusaidia mama kujifungua (suction machines) katika Zahanati ya Goba iliyoko Manispaa ya Ubungo ikiwa ni mchango kwa jamii.
Mganga mkuu Manispaa ya Ubungo  Peter Nsanya akizungumza na wanachama wa Goba Roads Runners(GRR), wauguzi wa zahanati ya Goba wakati wa kukabidhiwa kwa vifaa vya afya kwenye kituo hicho cha afya vilivyotolewa na uongozi wa Goba Roads Runners(GRR) ikiwa ni kurudisha mchango kwenye jamii.
Mwenyekiti wa bodi ya Goba Roads Runners(GRR) Fritz Msanjo akitolea ufafanuzi baadhi ya kazi zinazofanywa na Goba Roads Runners(GRR) hasa kwenye mchezo wa kukimbia pamoja na kushiriki kwenye jamii inayowazunguka wakati wa kukabidi vifaa tiba katika Zahanati ya Goba iliyopo Manispaa ya ubungo jijini Dar es Salaam.
Mganga mkuu Manispaa ya Ubungo Peter Nsanya akipeana mkono na Mwenyekiti Kamati ya Fedha wa Goba Roads Runners(GRR), Sulleiman Shermax mara baada ya kulipa pesa ya kuwa mwanachama wa Goba Roads Runners(GRR) wakati wa kukabidi vifaa tiba katika Zahanati ya Goba iliyopo Manispaa ya ubungo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wajumbe wa Goba Roads Runners(GRR), wauguzi na wanasiasa wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Mganga mkuu Manispaa ya Ubungo Peter Nsanya wakati wa kukabidhi vifaa tiba katika Zahanati ya Goba iliyopo Manispaa ya Ungungo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Goba Roads Runners(GRR), Revocatus Kahendaguza akitolea ufafanuzi baadhi ya mambo pamoja na kutambulisha wajumbe wa Goba Roads Runners(GRR) walifika kwenye Zahanati ya Goba kwa ajili ya kutoa msaada wa vifaa tiba kwenye Zahanati hiyo leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...