Rania Nasser ambaye ni Mwanafunzi wa Kidato cha Tano ameandaa maonyesho ya picha yanayojulikana kama 'Watu wa Tanzania' ambayo yatafanyika Alliance Francaise jijini Dar es Salaam tarehe 7 na 8 Agosti 2020.

Matumizi ya picha na video kuelezea stori au hadithi ni muhimu Sana, yanaelimisha, kubadilisha Habari za kuhadithiwa na muonekano pamoja na kuleta mabadiliko chanya kwa Dunia. Tumeona mfano mingi kwenye hili. Mabadiliko yanaanza kwa kubadilisha maono ya jamii.

Tangu akiwa na umri mdogo, Rania ametembelea sehemu mbali mbali za nchi yake Tanzania na sehemu zote hizo ambazo ametembelea na watu aliokutana nao, na Habari zile ambazo amezipata, ameona kilicho bora kwa Watanzania.

Rania pia ameweza kutembelea nchi zingine ulimwenguni lakini ukarimu na upole wa Watanzania umekuwa ni wa kipekee.Wakati wa kutembelea nchi hizo zingine, Rania ametengeneza marafiki wengi. Kitu kimoja ambacho ameweza kutambua ni kwamba wengi wanajua machache kuhusu Bara la Afrika, na Sana Sana Tanzania.

 Anasema 'naelewa ya kwamba kuna watu hawajui ya kwamba Afrika sio nchi, na hii sio kwa kila mtu, siwezi kupata picha kwa umasikini unaokumba vijiji vyetu, mapigano kwenye Miji yetu, magonjwa na mengine mengi'

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...