Wagombea Ubunge, Deo Ndejembi wa Chamwino na Livingstone Lusinde 'Kibajaji'  wa Mtera wakiwa katika picha ya pamoja kuelekea ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma leo.
 Wagombea wa Ubunge, Deo Ndejembi wa Chamwino na Livingstone Lusinde wa Mtera ambao wote wanatoka Wilaya ya Chamwino wakirudisha fomu zao kwa Msimamizi wa Uchaguzi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, Athuman Masasi.
 Wagombea wa Ubunge Livingstone Lusinde (kushoto) na Deo Ndejembi wakisaini fomu wakati wa kurudisha fomu za kuomba kuteuliwa kwa Msimamizi wa Uchaguzi ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, Athuman Masasi.
Mgombea Ubunge wa Chamwino, Deo Ndejembi akirudisha fomu za kuomba kuteuliwa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino ambaye ndie msimamizi wa uchaguzi, Athuman Masasi.

Charles James, Michuzi TV

BAADA ya kupitishwa na Chama chao cha Mapinduzi (CCM) na kisha kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa leo wagombea wa Ubunge, Deo Ndejembi wa Jimbo la Chamwino na Livingstone Lusinde 'Kibajaji' wa Mtera wamerudisha fomu kwa Msimamizi wa Uchaguzi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, Dodoma, Athuman Masasi.

Wagombea hao wote majimbo yao yapo katika Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma ambapo wameahidi kufanya kampeni za kistaarabu huku wakiahidi kushughulika na kero za wananchi.

Akizungumza baada ya kurudisha fomu mgombea wa ubunge Chamwino, Deo Ndejembi amesema anaamini kwa mambo makubwa yaliyofanywa na Rais Dk John Magufuli ni wazi watapata kura nyingi za ndio kutokana na imani kubwa ambayo serikali imejenga kwa wananchi.

" Nakishukuru chama changu kwa kunipitisha niwaahidi ndugu zangu wa Chamwino kwamba ninakuja kufanya kazi ya kuwatumikia nyinyi, ninakuja kushirikiana na serikali yetu kuwaletea maendeleo ya kijamii na kiuchumi," Amesema Ndejembi.

Kwa upande wake Lusinde amewataka watanzania kumpigia kura nyingi za ndio Rais Magufuli ili kumpa heshima kwa utendaji wake uliovunja rekodi nchini na nje ya Nchi.

" Wananchi wenzangu wa Chamwino ni ahadi yetu kwenu kwamba tuna dhamira ya dhati ya kuwatumikia, mmeona namna ambavyo Rais wetu amefanya kazi kubwa ikiwemo kuifanya Nchi yetu kuwa na uchumi wa kati hata kabla ya 2025 ambapo tulikua tumejiwekea malengo," Amesema Lusinde.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...