Na.Vero Ignatus
Kufunga mkanda kupo kwa mujibu wa sheria ukiangalia kwenye Kifungu no.11 sura 168 katika sheria za usalama barabarani,inamtaka wakati wote dereva,abiria kufunga mkanda na siyo vinginevyo,kufunga mkanda katika matumizi ya chombo cha moto ni jambo la lazima kwa matakwa ya kisheria,kwamba mtu yeyote yule anayekuwepo ndani ya gari inamlazimu kufunga mkanda kwaajili ya usalama wake.
Solomon Mwangamilo ni mkuu wa Kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Arusha anasema :Magari ya abiria yanatakiwa yawe na mikanda ndiyo maana tunafanya kaguzi kila siku, kuhakikisha kwamba inafanya kazi ,lakini inatumiwa ipasavyo na watu wanaosafiri na magari ,mikanda husaidia kwa asilimia 60%70% pale gari linapopata ajali,tofauti na ambaye hajafunga mkanda
''Magari ya abiria yote yanatakiwa yawe na mikanda ,wakumbusheni abiria mara kwa mara kwamba kuna kufunga mikanda ,japokuwa wapo abiria wengine hawataki kufunga mikanda, ni kwasababu tu inaonekana mikanda inawakera ila watambue kuwa ndiyo usalama wao kwa asilimia 60%70% usifunge mkanda kwa kumuogopa polisi ''.Alisisitiza Mwangamilo.
Anasema kuwa wapo baadhi ya madereva ambao wanaendesha magari bila kufunga mkanda,mara anapomuona askari wa usalama barabarani ndipo anatafuta mkanda ulipo,wanapeana ishara na madereva wenzao kwamba funga mkanda askari wapo mbele ,hiyo ni kuidanganya nafsi wanajiweka kwenye eneo la hatari pale inapotokea tafrani yeyote ya ajali
Anaendelea kusema kuwa Watoto wadogo chini ya miaka 5-8 size ya mkanda inaweza isimtoshe, haishauriwi mtoto kukaa katioka kiti cha mbele ,wanatakiwa wawekwe kiti cha nyuma, labda uwe na kiti chake maalum na kifungwe vizuri kwa matumizi ya mtoto.
''Usimuweke mtoto kiti cha mbele kwa kumfurahisha ,mchelea mwana kulia hulia wewe,kwenye kiti cha mbele kuna risk kubwa ikitokea dharura ya aina yeyote brekak za ghafla mtu anaweza kupita hata kwenye kioo cha mbele,kupasuka tairi n.k''Alisisitiza RTO Mwangamilo
Mwenyekiti wa Taasisisi isiyo ya Kiserikali ya Salama Salmini Foundation, Alhaj Muhammad Shaban (Aluta) anasema:Mikanda ya Usalama kwenye gari vimetengenezwa kuwaweka watu katika viti vyao na kuwalinda panapotokea ajali ili kuzuia au kupunguza majeraha.
Anaongezea na kusema:Mikanda ya Usalama hupunguza sana hatari ya kutupwa nje ya gari, hivyo basi ni muhimu sana Dereva, Abiria ikiwemo wale vya viti vya nyuma wafunge mkanda kila mara wanaposafiri hata kama ni safari fupi na watoto chini ya miaka 12 wawekwe kwenye viti maalumu vya usalama kwenye viti vya nyuma
Aidha Tasisi hiyo inayo wanaendesha Kampeni ya Mtandaoni ya #FungaMkandaChallenge ni kampeni ya kuhamasisha dereva na abiria kufunga mkanda wawapo safarini
Fatuma Emmanuel (37)mkazi wa Siha Snya juu ,anasimulia kisa cha ajali aliyoipata Moshi mkoani Kilimanjaro july 2017, majira ya saa mbili kasoro usiku: Ndani ya gari aina ya tulikuwa watu 4 wote tulikuwa tumefunga mikanda,tulipokaribia keep left ya ya kwanza ili tukakutane na ile ya YMCA, nilimuona dereva anaaza kuhama kutoka upande wa kushoto wa barabara kuelekea kulia ,ghafla nikasikia mmoja wetu akisema usimkwepe huyo mgonge..........
Ndipo niliposhtuka kuangalia mbele alikuwa amekaribia kugonga bodaboda iliyopakiza watu watatu mshikaki,ghafla gari lilikosa muelekeo kwani dereva alikuwa katika mwendo kasi ,gari ilianguka na ikaanza kubimbirika kama mara 4 hivi maana eneo lile lilikuwa na mteremko.
Hatimaye gari ilienda kujikita pembezoni mwa ukuta wa barabara,ndiyo ilikuwa salama yetu,wote tulitoka salama kwasababu tulikuwa tumefunga mikanda, japokuwa gari yetu iliharibika sana ila sisi tulikuwa salama, nasema hayo ili ndugu zangu muone umuhimu wa kufunga mkanda muda wote uwapo safarini.Anasema Fatuma Eammanuel
Mikanda ya usalama ni muhimu japo kuwa mara nyingi madereva hawaitilii maanani kulingana na Tim Hurd msemaji wa Wizara ya Uchukuzi nchini Marekani anasema kwamba mkanda wa usalama ndiyo njia yenye matokeo zaidi ya kuokoa maisha katika ajali.
Anasema abiria mwenye umri mdogo zaidi kiwango cha kuokoka kinakuwa karibu mara tatu kwa kutumia viti vya usalama vya watoto
Uchunguzi unaonyesha kuwa theluthi moja ya wenye kusafiri katika magari ya abiria katika nchi ya marekani hawatumii mikanda ya usalama ya viti
Ajali za barabarani zinaacha yatima, wajane, wagane, na kuleta simanzi kubwa katika familia, zinavunja ndoa, vinatenganisha familia, zinaleta au kuongeza umasikini katika familia,zinafifisha ndoto za watoto na vijana,ni chanzo cha ulemavu mwingi wa ukubwani duniani.
Taarifa hizi ni muhimu kuzifahamu katika maisha ya kila siku juu ya ajali za barabarani kwamba: maisha yako, viungo vyako havina spea; ukishakufa umekufa, ukishapoteza mguu, huwezi pata mguu mwingine kama uliokuwa nao awali.
Sheria ya usalama barabarani ya mwaka 1973, ambayo ilifanyiwa marekebisho mwaka 2002, nchini Tanzania ina mapungufu ambayo kwa namna moja ama nyingine, hukwamisha mpango wa kutokomeza ajali za barabarani pamoja na madhara yake.
Kwa mfano sheria hiyo ya usalama barabarani ya mwaka 1973 na kufanyiwa marekebisho 2002, imewasahau abiria wanaokaa viti vya nyuma kutokufunga mkanda,kwa mujibu wa kifungu hichi dereva na abiria wa mbele ndio wanatakiwa kufunga mkanda huku wale waliokaa nyuma wakiachwa huru
Tafiti zinaonyesha kuwa nchini Marekani ajali za magari ndizo kisababishi kikuu cha vifo miongoni mwa vijana hadi miaka 24,nchini japani ajali husababisha vifo mara mbili ya kansa ya matiti na kuua mara 4 zaidi ya saratani ya tezi dume,Ulaya ajali husababisha vifo vya watu mara nne zaidi ya uuaji wa kimakusudi.
Wataalam wa usalama wanadai kuwa ajali 9 kati ya 10 zingeweza kuzuiwa au kuepukwa kwa kudhibiti kikomo cha mwendo kilichotakiwa barabarani kupindapinda kwa magari,kukaribiana kupita kiasi,dereva kuendesha akiwa amelewa huku hajafunga mkanda.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...