Katibu Mkuu Wizara ya Afya-Idara Kuu ya Maendeleo ya Jmaii Dkt. John Jingu akizungumza na mmoja wa watoto wanaolelewa katika Kituo cha Malezi cha Nyerere, Igombe Jijini Mwanza.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya-Idara Kuu ya Maendeleo ya Jmaii Dkt. John Jingu akikagua baadhi ya miundombinu katika Kituo cha Malezi na Makuzi ya awali ya mtoto cha Nyerere, Igombe Jijini Mwanza.Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW

…………………………………………………………………………….

Na Mwandishi Wetu Mwanza

Serikali kupitia Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii kuanzisha Vituo vya Malezi na Makuzi ya awali kwa watoto wenye umri kati ya miaka mitatu na minne nchi nzima, ikiwa ni moja ya mikakati ya kumjenga na kumlinda mtoto

Kauli hii imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya-Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu alipofanya ziara katikaituo cha malezi na makuzi ya awali ya Mtoto cha Nyerere kilichoko Igombe Ilemela jijini Mwanza.

Dkt. Jingu amesema Vituo vya malezi na Makuzi kwa watoto ni muhimu sana ili kuhakikisha wanapata huduma bora zitakazowezesha uchechemuzi wa bongo zao kuwekwa katika mazingira mazuri ya ukuaji. “Hivi ni vituo muhimu unaweza ukadhani ni jambo dogo, hili ni jambo kubwa sana na la msingi katika malezi na makuzi kwa watoto wetu” alisema

Ameongeza kuwa vituo hivyo vitani suluhisho tosha kwa tatizo la malezi na makuzi ya mtoto hasa kwa changamoto za utafutaji kipato kwa wazazi kukosa muda mwingi wa asubuhi mpaka jioni kukaa na watoto wao.

“Vituo vya malezi na makuzi ya awali kwa watoto vinalenga kutoa fursa kwa wazazi na walezi kutekeleza shughuli za kiuchumi” alisema

Naye Afisa Mradi Kituo cha Malezi na Makuzi cha Nyerere Julieth Joseph amesema kuwa Kituo cha Malezi na Makuzi ya Mtoto cha Nyerere kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2016 mpaka mwaka 2019 kimefanikiwa kuwaandaa watoto zaidi ya 400 kabla ya kuwapeleka katika Shule za awali.

“Walimu katika Shule tulizowapeleka watoto hao wanasema watoto wanaopatia katika Kituo hiki wanakuwa na uelewa wa haraka ukilinganishwa na watoto amabao hawajapitia katika vituo vya malezi” alisisitiza Ameongeza kuwa ujifunzaji kwa watoto umezingatia falsafa za malezi na makuzi ya mtoto zinazohimiza umuhimu wa miaka ya mwanzo ya mtoto kupata uangalizi na malezi bora kwani ni msingi wa maisha ya baadaye

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...