MGOMBEA Ubunge jimbo la Mkuranga,Abdallah Hamisi Ulega anatarajia rasmi kurudisha fomu kesho baada ya udhamini ukamilika. 

Akizungumza wilayani Mkuranga mkoani Pwani leo Agosti 24, 2020  baada ya kumaliza kujaza fomu Ulega amewashukuru wote waliomdhamini na kuahidi kutokuwangusha. 

Aidha ametoa wito kwa wanachama  wa Chama cha Mapindunzi kuhakikisha wanashiriki kampeni kikamilifu ili kuwezesha chama hicho kushinda kwa kishindo. 

Pamoja na kuwashukuru waliomdhamini Ulega amewahidi kutowaangusha wanamkuranga na kuwataka kuendelea kudumisha umoja na ushirikiano ndani na nje ya chama. 

Zaidi ya wadhamini mia 300  wamejitokeza kumdhamini Ulega huku wanaohitajika  ni thelasini na moja tu. 
Mgombea Ubunge jimbo la Mkuranga, Abdallah Hamisi Ulega (kushoto) akizungumza na wanachama wa Chama cha Mapindunzi  baada ya kumaliza kujaza fomu  ya kugombea ambapo amewashukuru wote waliomdhamini na kuahidi kutokuwangusha, leo Agosti 24, 2020  wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.
Wanachama wa Chama cha Mapindunzi  wakimsikiliza Mgombea Ubunge jimbo la Mkuranga,Abdallah Hamisi Ulega (hayupo pichani)
Mgombea Ubunge jimbo la Mkuranga,Abdallah Hamisi Ulega akiwasalimia Wanachama wa Chama cha Mapindunzi.
Mgombea Ubunge jimbo la Mkuranga,Abdallah Hamisi Ulega akiwasalimia Wanachama wa Chama cha Mapindunzi.
Mgombea Ubunge jimbo la Mkuranga,Abdallah  Hamisi Ulega (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa  Chama cha Mapindunzi (CCM) leo Agosti 24, 2020  wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...